Page 128 - Arabic_F5
P. 128
Form Five
:ةجرـَّ تلا
ََ
ُ
ْ
Afrika kwa sasa inajumuisha nchi huru hamsini na nne. Nyingi ya nchi hizi bado
ziko kwenye mipaka iliyowekwa tangu enzi za ukoloni. Idadi kubwa ya nchi hizi
FOR ONLINE READING ONLY
ni jamhuri zinazofanya kazi chini ya aina fulani ya mfumo wa rais wa serikali.
Licha ya hayo, wachache wao wameweza kudumisha mifumo ya utawala
inayoungwa mkono na demokrasia. Hii ni kwa sababu wengi wao walipitia
msururu wa mapinduzi yaliyopelekea udikteta wa kijeshi. Jeshi lilionekana kuwa
kundi pekee ambalo lingeweza kufanya kazi kwa ufanisi katika kudumisha
utulivu. Lakini halikufanikiwa katika hilo; Ubaguzi wa kikabila, migogoro ya
vyeo, na ufisadi ni miongoni mwa sababu kuu za kurudi nyuma na kukosekana
kwa utulivu wa ndani.
ِ
ِ
ِ
ِ
ِ
ِ
ِ
ِ حا َ ن ىدم حضوو ةَّ ييِ وْ قـت ةَّ يدْ قـن ً ةءارق ت ْ لا َّ صَّ نلا أرـْ قا :2 بيردَّ تلا
ْ
ً ْ َ ً
َ
ّ
ُ ْ
َ
َ
َ
َ ْ ََ
َ َ َ
ِ
ِ
:مجرـتمْلا
ْ َُ
:ُّ صَّ نلا
Shaaban Robert alizaliwa Tanga tarehe 1 Januari, 1909. Alipata umaarufu
mkubwa katika taaluma ya fasihi na lugha ya Kiswahili katika bara la Afrika na
dunia kwa ujumla. Aliandika fani nyingi za fasihi ya Kiswahili ikiwemo mashairi,
riwaya, tamthilia. Inaonekana wazi kuwa hadi leo hakuna mtu aliyekitumikia
Kiswahili zaidi yake. Alitumia umahiri wake wa kilugha hasa ushairi katika
harakati za kupigania uhuru. Maandishi yake yalibeba maudhui za utu, nafasi ya
mwanamke katika jamii, ukombozi wa Afrika, kukuza lugha ya Kiswahili, na
maendeleo. Akiwa ameshafariki alitunukiwa tuzo ya fasihi iliyotukuka kutokana
na mchango wake katika kuitumikia jamii ya Tanganyika na Tanzania kwa jumla.
Shaaban Robert alifariki tarehe 20 Juni, 1962 kwa maradhi ya moyo na upungufu
wa damu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu gwiji huyu wa fasihi ya
Kiswahili na amlaze mahala pema peponi, amin.
121 Arabic for Advanced Secondary Schools Student’s Book Student’s Book
30/06/2024 17:58
ARABIC LANGUAGE FORM FIVE.indd 121 30/06/2024 17:58
ARABIC LANGUAGE FORM FIVE.indd 121