Page 137 - Arabic_F5
P. 137
Form Five
ِ
ِ ِ
ِ
ِ
ِ ِ
ِ
ِ
ِ
ِ
ِ ِ
:ةَّ يبرعْلا َ لإ تلا َّ صَّ نلا مجرت ةَّ يجوُ لوـنْ كتلا لئاسوْلا مادـخـتـسب :2 بيردَّ تلا
ْ
ُْ ّ
ُ ْ
َ ْ ْ
ََ
َ َ
َ
Biashara ndogondogo ni muhimu sana nchini Tanzania. Wawekezaji
wadogowadogo hutoa asilimia kubwa ya ajira nchini, na ni wachangiaji muhimu
FOR ONLINE READING ONLY
katika pato la taifa. Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba upanuzi wa sekta binafsi kupitia
biashara ndogondogo ni muhimu kwa utoaji wa nafasi za kazi na ukuaji wa
uchumi nchini. Ustawi wa nchi yetu unategemea ukuaji wa biashara hizi, kupitia
kwazo riziki hupatikana kwa njia halali.
Kuna fursa kubwa kuziendeleza zaidi biashara hizi; kwani idadi ya watanzania
kwa sasa ni zaidi ya milioni 61. Hata hivyo, gharama za uendeshaji wa biashara
ni kubwa kutokana na upungufu wa miundombinu ya kuinua uwekezaji.
Miundombinu ya uchukuzi haitoshi na upatikanaji wa mitaji bado ni changamoto.
Biashara nyingi ndogondogo zinahitaji fedha zaidi ili ziweze kukua, lakini isivyo
bahati mikopo ya benki ni ghali sana; kwa sababu ya viwango vya juu vya riba.
Katika mazingira hayo, biashara chache sana zinaweza kufanikiwa kutimiza
malengo yake. Kwa hiyo, tunaiomba serikali itoe msaada zaidi kwa wafanya
biashara wadogowadogo kwa lengo la kukuza harakati za kiuchumi nchini.
ِ
ِ
ِ ِ ِ
ِ ِ
ِ
ِ ِ
ِ
ِ
َ لإ تلا َّ صَّ نلا مجرـت ةَّ يجوُ لوـنْ كتلا لئاسوْلا مادـخـتـسب :3 بيردَّ تلا
َ ْ
ْ
َ َْ ُْ ّ َ َ ْ ُ ْ
ِ
ِ
:ةَّ يبرعلا
ََ
Baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia kumalizika, mataifa yaliunda
chombo ambacho kilitarajiwa kuleta umoja na kudumisha amani duniani. Kwa
upande mwingine, sehemu iliyokuwa ikitawaliwa na Wajerumani Afrika
Mashariki iligawanywa na kupatikana nchi tatu, ambazo ni Tanzania, Kenya na
Uganda, na kuwekewa mipaka ipasavyo. Pamoja na Waingereza kuitawala Kenya
kama koloni lao, pia walikabidhiwa madaraka ya kuisimamia Tanganyika kwa
niaba ya umoja huo. Mwaka 1939 vilizuka Vita vya Pili vya Dunia wakati
Waingereza wakiwa bado ni wasimamizi wa Tanganyika. Kiuhalisia, Wajerumani
walikalia ardhi ya Tanganyika kwa kipindi cha miaka 27 na Waingereza kipindi
cha miaka 42, jumla ya miaka 69 taifa lilikuwa chini ya wakoloni.
Student’s Book Student’s Book Arabic for Advanced Secondary Schools 130
30/06/2024 17:58
ARABIC LANGUAGE FORM FIVE.indd 130
ARABIC LANGUAGE FORM FIVE.indd 130 30/06/2024 17:58