Page 122 - EDK_F5
P. 122
SURA YA TATU NGUZO ZA IMANI
Kwa kuweka bayana suala kama hili aliulizwa Mtume Muhammad (S.A.W) kwa kuwa
Allah (S.W) kishakadiria kila kitu ipo haja ya kufanya amali? Akajibu katika Hadith
ifuatayo:
Kutoka kwa Ali (R.A), amesema: “Siku moja Mtume wa Mwenyezi
Mungu (S.A.W) alikuwa amekaa, na mkononi mwake alikuwa na fimbo
FOR ONLINE READING ONLY
akaigonga ardhini kwa nguvu, akainua kichwa chake na kusema:
Hakuna nafsi yoyote kati yenu isipokuwa inajulikana mahala pake baina
ya Pepo na Moto, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa
nini sasa tunafanya Amali? Hivi hatukai tu (tukaacha amali)? Akasema:
Hapana, fanyeni, kwani kila mtu amerahisishiwa yale aliyoumbiwa
kwayo, kisha akasema: Yule anayetoa (zaka, sadaka na vingenevyo)
na kumcha Mwenyezi Mungu. Na kusadiki jambo jema (akalifuata).
Tutamsahilishia njia ya kwenda Peponi. Na afanyiaye ubakhili, viumbe
wenzake. Na akakadhibisha (asiyafanye) asiwe na haja ya mambo
mema. Tutamsahilishia njia ya kwendea Motoni. (Bukhari na Muslim).
Kwa hiyo, mja atakapofanya maasi kama kuacha kuswali, kuzini, kunywa ulevi na
mengineyo basi ataandikiwa dhambi na kuadhibiwa kwa kuwa kayafanya kwa hiari yake
bila ya kulazimishwa.
Pili, Kutoamini Qadari inapelekea kutokamilika imani ya mja na kuwa kafiri, kama
ilivyokuja katika Hadith ya Mtume Muhammad (S.A.W):
Kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu
(S.A.W) amesema: “Hakuna mja mwenye imani mpaka aamini Qadari za
kheri na shari zake, mpaka ajue kwamba lililompata halikuwa limkose,
na lile alilolikosa halikuwa alipate”. (Tirmidhy na Ahmad).
112