Page 123 - EDK_F5
P. 123
SURA YA TATU NGUZO ZA IMANI
Zoezi la 3 1
Jibu maswali yafuatayo kwa ufupi
1. Soma aya ifuatayo kisha eleza aya hiyo inahusu jambo gani
FOR ONLINE READING ONLY
َ
ۡ ۡ
َ
َ َ
ٓ
َ
ۡ َ
َ َ
َّ
ۡ ۡ
َ ُّ َ َ
َ ۡ
َ َ
َ
َ َ ً
َ ُ َ
َّ
َ
َ َ
ۡ
ٰ
ٰ
ٰ
ٰٓ
قلتف رخاء اهلِإ ِللٱ عم لعت لو ِۗةمكِلٱ نِم كبر كلِإ حوأ امِم كِلذ
ً ُ ۡ َّ ٗ ُ َ َ َّ َ َ
٣٩اروحدم امولم منهج ِ ف
Haya ni katika yale aliyokufunulia Mola wako katika hikima (zake).
Wala usimueke pamoja na Mwenyezi Mungu, mungu mwengine, usije
kutupwa katika Jahanamu hali ya kuwa mwenye kulaumiwa (na)
mwenye kufukuzwa (huku na huku). (Israa, 17:39)
2. Eleza dhana ya uungu kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’an
3. Fafanua maana ya kuamini Qadar ya Allah (S.W)
4. Onesha namna mtazamo potofu juu ya Qadar unavyoathiri jamii yako
Ufupisho
Allah (S.W) ameumba ulimwengu na vilivyomo ikiwa ni dalili ya kuwepo kwake na
Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa. Imani ya mja haikamiliki mpaka aamini nguzo
sita za imani ambazo zinategemeana, na kama mtu atakanusha moja katika hizo basi
mtu huyo atakuwa kafiri na ataadhibiwa siku ya Kiyama.
Mja anapoamini nguzo sita za imani hupata athari kubwa katika utekelezaji wa amali
zake, na humpelekea kwenye uchamungu na hatimaye kupata malipo mema kwa
kuingizwa peponi.
Ama kwa wale wenye matazamo potofu wa kuamini nguzo hizo basi unawapelekea
kukanusha nguzo hizo na kuwa ni miongoni mwa watu waliopotea na kupata hasara
kubwa, na malipo yao ni motoni.
113