Page 82 - EDK_F5
P. 82
SURA YA TATU NGUZO ZA IMANI
ُّ َ َ َ ٗ ُ َ َ ۡ ۡ َ َّ ُ َ ُ َ َّ َ َ
ٰ
ٰ
٨يرِنم بتِك لو ىده لو ملِع يرغب ِللٱ ِ ف لِدجي نم ِ سالنٱ نِمو
ِ ِ
ٖ
ٖ
ٖ
Na katika watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya
ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru. (Al-Hajj, 22:8).
َ
َ
َ
ۡ ُ ۡ َ َ َ ۡ َ َ ۡ َ َ َ َ َّ َّ ُ َ َ َّ َ َ َّ َّ َ ْ ۡ َ ۡ َ َ
ٰ ٰ
مكيلع غبسأو ِ ضرۡلٱ ِ ف امو ِ تومسلٱ ِ ف ام مكل رخس للٱ نأ اورت ملأ
FOR ONLINE READING ONLY
ٗ
ٗ ُ َ َ ۡ ۡ َ َّ ُ َ ُ َ َّ َ َ َ َ َ ٗ َ َ ُ َ َ
ٰ
ٰ
ىده لو ملِع يرغب ِللٱ ِ ف لِدجي نم ِ سالنٱ نِمو ۗ ةنِطابو ةرهظ ۥهمعِن
ٖ
ِ
ِ ِ
ُّ َ َ َ
ٰ
٢٠يرِنم بتِك لو
ٖ
ٖ
Kwani hamwoni ya kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya vikutumikieni
viliomo mbinguni na kwenye ardhi, na akakujalizieni neema zake, za
dhaahiri na za siri? Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu
ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye
nuru. (Luqman, 31:20)
Kwa mujibu wa aya hizi inadhihirika suala la kumuamini Allah (S.W) na kumuabudu
ipasavyo ni suala linalohitajia elimu na wale waliozama katika elimu ndio
wanaomyakinisha na kumuabudu Allah (S.W) kwa upeo zaidi. Rejea Qur’an Fatir,
35:27-28).
Tano, mitume waliletwa kwa dalili zinazothibitisha kuwepo kwa Allah (S.W). Mitume
walilingania watu juu ya Allah (S.W) kwa kutumia dalili mbali mbali na vitabu vya Allah
(S.W) walivyoshushiwa.
ۡ
َ
ۡ
َ ُ َ َ َ ۡ َ َ َ ۡ ُ ُ َ َ َ َ َ َ َ ّ َ ۡ َ ُ ُ َ َ ۡ َ ۡ َ َ
ٰ
ٰ
موق ِ ل نايزِملٱو بتِكلٱ مهعم النزنأو ِ تنيلٱب انلسر انلسرأ دقل
ِ
ِ
ۡ
َ
ۡ
َ
َ ۡ َ َّ ُ َ َ َ ٞ َ ٞ َ َ َ ۡ َ َ َ ۡ ۡ ُ َّ
َ
ٰ
ملع ِ لو ِ سانلِل عِفنمو ديِدش سأب ِهيِف ديِدلٱ النزنأو ِۖ طسِقلٱب سالنٱ
ِ
َ
َ
ٞ َ ٌّ َ َّ َّ ۡ َ ۡ ُ ُ ُ َ ُ ُ ُ َ َ ُ َّ
٢٥زيزع يوق للٱ نِإ بيغلٱب ۥهلسرو ۥهصني نم للٱ
ِۚ
ِ
ِ
ِ
Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na
tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu,
na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na
ili Mwenyezi Mungu amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wake kwa
ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.
(Al-Hadid, 57:25).
Hivyo, hoja hizi tano zinathibitisha kwamba kumuamini Allah (S.W) si suala la kibubusa.
Kwani kupitia tafakuri, hoja, elimu na utafiti, Allah (S.W) anaweza kubainika kupitia;
umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake, nafsi ya mwanadamu, historia
ya mwanadamu, maisha ya mitume pamoja na mafundisho ya mitume.
72