Page 202 - EDK_F5
P. 202
SURA YA SABA UTEKELEZAJI WA NGUZO ZA UISLAMU
(R.A), aliwapiga vita watu wa Yamama kwa kukataa kutoa zaka, kwani alisema hakuna
kutofautisha baina ya nguzo ya swala na nguzo ya zaka.
Katika utekelezaji wa nguzo ya Hijja, pia hutekelezwa nguzo nne zilizobakia,
Mahujaji, wawapo katika viunga vya Makka, wakitekeleza nguzo ya Hijja, takribani
FOR ONLINE READING ONLY
huwa wanatekeleza pia nguzo zote za Uislamu. Yaani, wanatamka shahada kwa kukariri
mara kwa mara, wanaswali, wanatoa zaka na wanafunga hasa kwa mtu aliyevunja miiko
ya hijja, anapaswa afunge siku 10, tatu akiwa hijja na saba akirejea nyumbani kwao.
Hii ni ishara kwamba nguzo za Uislamu zina uhusiano mkubwa katika utekelezaji wake.
Hujaji anapofunga safari kwa ajili ya Hija, huwa tayari kutengana na familia yake,
ndugu, jamaa na rafiki zake kwa kipindi chote cha safari na huwa tayari kukabiliana na
misukosuko na magumu yote ya safari na huwa tayari kufuata barabara masharti ya Ihram
na masharti yote ya hijja kwa ujumla kwa ajili tu ya kutafuta radhi za Allah (S.W). Pia,
Hija inamzoesha Muislamu kuwa tayari kujitoa muhanga kwa mali yake na nafsi yake
kwa ajili ya kusimamisha dini ya Allah (S.W). Kwa mawanda ya kijiografia nguzo hii ndio
nguzo kubwa kwa maana hubeba uhalisia wa mahusiano ya Waislamu kimataifa, wakiwa
na sare moja (Ihram), lugha moja, hotuba moja (Arafa) , na matendo yote hufanyika kwa
hali ya usawa bila matabaka ya rangi, kabila wala taifa.
Utekelezaji wa nguzo zote hujenga uhusiano wa karibu wa mja na Allah (S W)
pamoja na viumbe vyake, mwanadamu anapaswa kujenga uhusiano mzuri baina yake
na Mola wake Mlezi na baina yake na viumbe vya Mola wake. Uhusiano wote wa aina
mbili hujengeka kwa kutekeleza nguzo za Uislamu. Kwanza, shahada inamuunganisha
mja na Mola wake kwa kukataa kumuabudu yeyote kati ya viumbe vyake ila Yeye tu. Pili,
swala humkataza mja na maovu na machafu, kwa kukatazika huko atakuwa na uhusiano
mzuri na Mola wake Mlezi pamoja na jamii inayomzunguka kwa kuwa na tabia njema.
Tatu, zaka inayolenga kutakasa nafsi ya mtoaji, mali ya mtoaji na jamii ya Kiislamu,
inajenga uhusiano mwema baina ya mtoaji na Mola wake, na mtoaji na jamii yake. Nne,
Saumu inayomwandaa mja kuwa mchamungu pia inaleta uhusiano imara kati ya mfungaji
na Mola wake na mfungaji na jamii yake, kwani mchamungu huwa na tabia na mwenendo
mzuri unaoridhiwa na Mola wake Mlezi pamoja na unaokubalika na jamii yake. Tano,
hijja inayomuandaa Hujaji kumtumikia Mola wake Mlezi, nayo ina nafasi kubwa katika
kuibua uhusiano baina ya hujaji na Mola wake, na Hujaji na jamii yake, kwani hujaji
hana hiari ila kutii maamrisho na kuacha makatazo ya Allah (S.W), jambo ambalo huleta
uhusiano mwema baina yake, Mola wake na viumbe wa Allah (S.W).
192