Page 204 - EDK_F5
P. 204
SURA YA SABA UTEKELEZAJI WA NGUZO ZA UISLAMU
Itikadi, katika sharti hili humtaka anayetekeleza nguzo za Uislamu itikadi yake iwe ni
Uislamu na ndio maana katika kuzipanga nguzo za Uislamu, Shahada inachukuwa nafasi
ya kwanza kama msingi wa utekelezaji wa nguzo nyingine. Kwa hiyo, hata kama mtu
ataamua kuswali usiku kucha, kufunga mwaka mzima au kutoa mali zake zote ikiwa
itikadi yake sio Uislamu basi hesabu zake zote zimepotelea patupu. Sharti hili huwagusa
FOR ONLINE READING ONLY
hata wale waliotamka shahada pindi wanapojiingiza katika shirki basi hubatilisha itikadi
yao na hivyo matendo yao pia hupeperuka.
Nia, sharti hili hulenga kusudio la ndani alilonalo Muislamu wakati wa kupanga na
kutekeleza jambo, linaweza pia kuitwa dhamira, dhumuni au msukumo wa ndani. Yaani
anafanya kwa ajili ya nini au kwa ajili ya nani na ili iweje. Kama ilivyoelezwa katika
mada tangulizi kuwa mwanadamu aliyetia nia ya kufanya ibada na akafanya kila juhudi
kukamilisha ibada hiyo na hakufanikiwa, basi hulipwa malipo sawa na yule aliyetekeleza
kwa ukamilifu. Funzo linalopatikana hapa ni kwamba mwanadamu amepewa uhuru wa
kuchagua kati ya kheri na shari, hivyo, ni juu yake kuamua. Kwa kuwa kiumbe huyu muda
mwingine anaweza kusema asichomaanisha, au kutenda na kusifia kile anachokichukia
moyoni basi Allah (S.W) ameepukana na udhaifu wa kuhadaiwa, hujua ya siri na dhahiri.
Japo mbele ya macho ya wanadamu mja huyu ataonekana mwema na atadhaniwa ni
mwenye kustahiki malipo makubwa, mbele ya Allah (S.W) ataonekana katika uhalisia
wake. Ndio maana imeelezwa kuwa siku ya kiyama watu watakimbiana kwa kuwa kila
mmoja yapo aliyoyafanya nafsi yake ikijua fika ni ria na hakukusudia kulipwa siku ya
hukumu:
Kutoka kwa Umar Ibn Al Khatwab (RA) ambaye amesema: Nilimsikia
Mtume wa Allah akisema: Bila shaka amali inategemea nia, na kila mtu
atapata kwa mujibu wa kile alichokinuia. Mtu ambaye hijra yake ni kwa
ajili ya Allah (S.W) na Mtume Wake (S.A.W), basi hijra yake ni kwa ajili
ya Allah (S.W) na Mtume Wake (S.A.W), Na ambaye hijra yake ni kwa
ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke, basi
hijra yake ni kwa lile aliloliendea. (Bukhari na Muslim)
Baadhi ya wanachuoni wamechukulia Hadith hii kuwa ni theluthi ya Uislamu; kwamba
muumini hulipwa kutokana na nia yake na uzuri wa amali yake, mwenye kuwa na matendo
mazuri na ikhlasi juu ya matendo hayo, atalipwa kutokana na usafi wa nia yake na ikhlasi
yake; na mwenye kufanya amali nzuri kwa kujionyesha kwa watu na si kwa ajili ya Allah
(S.W) basi amali hiyo itarejeshwa hata kama ni kubwa. Kwani sharti ya kukubaliwa amali
njema ni usafi wa amali hiyo na iwe ni kwa ajili ya Allah (S.W). Pia iwe imewafikiana
na mwongozo wa Mtume Muhammad (S.A.W).
194