Page 203 - EDK_F5
P. 203
SURA YA SABA UTEKELEZAJI WA NGUZO ZA UISLAMU
Zoezi la 7 1
1. Kwa kutumia mchoro ainisha uhusiano wa nguzo za Uislamu
2. Fafanua nguzo za Uislamu kwa kuzingatia lengo la kila nguzo
3. Shahada mbili ndio kiingilio cha Uislamu.Thibitisha
FOR ONLINE READING ONLY
4. Kwa kuzingatia utekelezaji wa nguzo za Uislamu, onesha uhusiano uliopo kati ya :
(a) Mja na Allah(S.W)
(b) Nguzo moja na nyingine
Uhusiano wa masharti, matendo na malengo ya nguzo za Uislamu
Kazi ya 7 2
Shirikiana na mwenzako chunguza uhusiano wa matendo na masharti ya Hija na nguzo
zingine za Uislamu kisha wasilisha kwa wanafunzi wenzako darasani
Katika utekelezaji wa nguzo za Uislamu takribani kila nguzo ina masharti na matendo
ambayo yakitekelezwa ipasavyo kwa mjumuiko wake, ndio hupelekea kufikiwa kwa lengo
la nguzo husika. Kwa kuwa mlengwa ni mmoja anayewajibika kutekeleza nguzo zote na
kama ilivyofafanuliwa hapo awali kuwa mlengwa huyu analo lengo la kuumbwa kwake
na nguzo hizi ni nyenzo tu zitakazo mfikisha katika ukamilifu wa lengo na hadhi. Kwa
ngazi hii ya Elimu ya dini ya Kiislamu, kipengele hiki kinafafanuliwa kwa muhtasari wa
kiuchambuzi kwani ngazi zilizotangulia kila nguzo ya Uislamu imechambuliwa kwa kina.
Masharti ni jumla ya mambo ambayo inamlazimu Muislamu ayatekeleze ili ibada husika
ikubaliwe. Katika kufafanua uhusiano wa masharti, yapo yanayojitokeza katika utekelezaji
wa kila nguzo na yapo masharti kwa baadhi ya nguzo kama ifuatavyo:
Utimamu wa akili, baleghe na Afya, ibada zote hufanywa kwa lengo la kuhitaji radhi
na malipo kutoka Allah (S.W). Hivyo katika mjumuiko wa watu wapo ambao hawana
wajibu wowote, kutokana na kukosa sifa ya sharti la utimamu. Watu hao ni pamoja na
mtoto mdogo hadi atakapofikia baleghe, mwenye kichaa au maradhi ya akili hadi akili
yake itakaporejea na vilevile mtu aliyelala usingizi atahesabika mwenye udhuru juu ya
utekelezaji wa ibada hadi atakapotoka usingizini. Katika Musnad Abu Hanifa kupitia
riwaya ya Al-Hasfiki kuna Hadith isemayo:
... Kalamu imezuiwa kwa watu watatu; mwenye kichaa mpaka arejewe
na akili, mtoto mdogo mpaka abaleghe na mtu aliyelala mpaka aamke.
193