Page 242 - EDK_F5
P. 242
SURA YA TISA HISTORIA KATIKA UISLAMU
Kwa maana,wengi wao si wenye kutimiza ahadi ipasavyo. Ishara ya kuasi ahadi zao ni
kule kuelekea katika upotofu na kwenda kinyume na mafundisho ya Mitume na vitabu
vilivyoteremshwa kwao.
Msimamo wa wanachuoni, tukio la ahadi ya utii limekubaliwa na kuungwa mkono na
FOR ONLINE READING ONLY
wanachuoni wa karne tatu bora za awali katika Uislamu. Kwa maana kila karne kuna
mwakilishi wa kuunga mkono kuwapo kwa tukio la ahadi hii, kwa mfano, karne ya
kwanza kulikuwa na Ibn Abbas, karne ya pili Sa’id Ibn Jubayr (aliyetawafu 95/714), na
al-Ḥasan al-Baṣri (aliyetawafu 110/728), ikifuatiwa na karne nyingine za baadaye. Hii ni
kwa kuwa ahadi hii ina uhusiano wa moja kwa moja na dhana ya fitra, au asili ya awali
ya mwanadamu, ambayo imetajwa katika Qur’an (30:30). Kwa mujibu wao, ahadi hii
inahusu wanadamu wote na kwamba kila mtu amezaliwa katika ulimwengu huu, akiwa
anatambua kuwa Allah (S.W) ndiye Mola wake na Mungu wa pekee.
Vikwazo vya kutekeleza ahadi ya utii
Ingawa mwanadamu ameahidi kumtii na kumwabudu Mola wake lakini kuna nguvu mbili
zinazosababisha kuasi ahadi yake katika maisha ya kila siku hapa duniani. Nguvu hizo
ni moja nguvu ya ndani na ya pili ni nguvu za nje ya nafsi yake. Vikwazo hivi aghalabu
hufanya kazi kwa kushirikiana, ingawa inaweza ikatokea kila kimoja kikafanya kazi peke
yake. Ufafanuzi wa vikwazo hivyo ni huu ufuatao:
Kwanza, matamanio ya nafsi. Hiki ni kikwazo kinachotokana na mwanadamu mwenyewe
nafsini mwake. Mwanadamu ameumbiwa matamanio na akatakiwa apambane nayo ikiwa
matamanio hayo yanamtoa katika utii. Ieleweke kwamba mwanadamu hana kosa kutamani
lakini suala ni kwamba anatamani nini? Anatamani yaliyo halali; ndoa, kula, kunywa
au kutembea? Au anatamani yaliyoharamishwa; zinaa, kamari, pombe au nguruwe?
Mwanadamu akitamani yaliyo halali, haingii katika uasi wa ahadi kwa sharti la kuwa
muda unaruhusu. Mfano kula ni halali lakini ikiwa mchana wa Ramadhan haruhusiwi.
Hivyo, ingawa kuna baadhi ya vitu ni halali lakini achunge vigezo na masharti. Kwa
upande wa kutamani yaliyo haramu, hii haikubaliki. Katika kutahadharisha kikwazo hiki
Qur’an inasema:
َ
ً َ ۡ َ ُ ُ َ َ َ َ ُ َ َ ُ َ َ َ َ َّ َ َ ۡ َ َ َ
َ
ٰ
ٰ
٤٣ ليِكو ِهيلع نوكت تنأفأ هىوه ۥههلِإ ذتٱ نم تيءرأ
ِ
Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake?
Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake? (Al-Furqaan, 25:43)
َ
َّ
ۡ َ َ ۡ َ َ َ َ َ َ َ ۡ َ َ ُ َّ ُ َ َ ُ َ َ ُ َ َ َ َ َّ َ َ ۡ َ َ َ َ
ٰ
ٰ
ٰ
ٰ
ۦِهبلقو ۦِهِعمس ع متخو ملِع ع للٱ هلضأو هىوه ۥههلِإ ذتٱ نم تيءرفأ
ِ
ٖ
ِ
َ
َ ُ َّ َ َ َ َ َ َّ ۡ َ ۡ َ َ ٗ َ َ َ َ َ َ َ َ َ
َ
ٰ
ٰ
ۢ
٢٣ نوركذت لفأ ِۚللٱ ِدعب نِم ِهيِدهي نمف ةوشِغ ۦِهصب ع لعجو
ِ
232