Page 243 - EDK_F5
P. 243
SURA YA TISA HISTORIA KATIKA UISLAMU
Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake,
na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na
akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika
vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya
Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki? (Al-Jaathiyah, 45:23)
FOR ONLINE READING ONLY
Yaani, ewe Mtume! Umemwona huyo mwenye kufanya matamanio yake ndiye mungu
wake wa kumuabudu, akamnyenyekea, na akamtii, na akaiacha Njia ya Haki na hali anaijua,
na akaziba masikio yake asisikie waadhi, na moyo wake asiamini Haki, na akabandika
vifuniko vya macho asione ya kuzingatiwa? Basi nani wa kumuongoa mtu huyu baada ya
kwishapuuzwa na Allah (S.W)? Je! Mnaacha kutazama ili msipate kukumbuka?
Pili, kikwazo cha wazazi au walezi. Kwa kuwa binadamu ni kiumbe kinachoathiriwa
na mazingira yake, athari hiyo inaweza kuwa mbaya au nzuri. Hivyo, wazazi au walezi
wanabeba nafasi kuwa katika kumkuza katika wema au uovu mtoto wao. Mitume peke
yao, ndio hawaathiriwi na mazingira yao, kwa kuwa Mola wao Mlezi amewakinga na
athari hizo za kimazingira. Imepokewa katika Muwatta Malik (1/393) kuwa:
“Kila mtoto huzaliwa katika umbile la fitra, basi wazazi wake
wanamgeuza kuwa Myahudi, au wanamgeuza kuwa Mkristo...”
Naam, hiyo ndiyo kazi inayofanywa na wazazi au walezi wa mtoto katika kumfanya aasi
ahadi yake kwa Muumba wake, nacho ni kikwazo cha pili kati ya vikwazo vitatu.
Tatu, shetani. Shetani ni kikwazo kikubwa katika kumchochea mwanadamu aasi ahadi yake.
Hii ni kwa sababu shetani ana nguvu mno ukilinganisha na vikwazo vilivyotangulia. Kuna
shetani wa kijini na wa kibinadamu. Yaani, shetani ni mazingira yote yanayompumbaza
mwanadamu katika kutekeleza ahadi yake. Katika kitabu cha Sharhu Mushkal Athar
(10/5) kuna Hadith Qudsi isemayo:
Hakika Nimewaumba waja Wangu wote Hunafaa (wapwekeshaji),
lakini waliwajia mashetani na wakawatenga na dini yao, wakawakataza
nilichoruhusu, wakawamrisha wanishirikishe na mambo ambayo
hawana ujuzi nayo.
Uhusiano wa ahadi ya utii na ahadi nyingine
Ahadi hii ya utii ina uhusiano na ahadi nyingine zilizotajwa katika aya za Qur’an, ingawa
kila ahadi ilikuwa na muktadha na wahusika wake. Ahadi hii ya utii iliwahusisha wanadamu
tu pasi na kiumbe kingine chochote. Allah (S.W) aliahidiana na mwanadamu na kufunga
mkataba wa kwamba binadamu atatii kila atakaloamrishwa na Mola wake Mlezi wakati
Mola Mlezi aliahidi kumruzuku kiumbe wake. Ufuatao ni uhusiano wa Ahadi ya Utii na
ahadi nyingine katika Qur’an:
233