Page 245 - EDK_F5
P. 245
SURA YA TISA HISTORIA KATIKA UISLAMU
Kufanana kwao, ahadi hii ya Mitume inafanana na Ahadi ya Utii katika lengo kwani
ingawa iliwahusu Mitume tu katika kufikisha ujumbe wa Allah (S.W) lakini ililenga
kuwakumbusha wanadamu kutekeleza ahadi yao ya utii, jambo ambalo ndilo lengo la
Ahadi ya Utii. Kutofautiana kwao, zinatofautiana katika wahusika, Ahadi ya Mitume
iliwekwa baina ya Allah (S.W) na Mitume, wakati Ahadi ya Utii, iliwekwa baina ya Allah
FOR ONLINE READING ONLY
(S.W) na wanadamu wote.
Tatu, Ahadi ya waumini kwa Allah (S.W). Ahadi hii iliwekwa baina ya waumini na Mola
wao Mlezi. Msingi wake ni kutekeleza mapambano baina ya haki na batili, ili uadilifu
usimame katika mgongo wa dunia. Qur’an inaliweka wazi hili na kusema:
َ
ُ ۡ َ ُ َ ۡ َ َ َ َّ ُ ۡ َ ۡ َ َ َّ ْ ُ َ َ َ ْ ُ َ َ ٞ َ َ ۡ ُ ۡ َ ّ
ٰ
ٰ
مهنِمو ۥهبن ضق نم مهنِمف ۖ ِهيلع للٱ اودهع ام اوقدص لاجر ينِنِمؤملٱ نِم
ِ
ٗ ۡ َ ْ ُ َّ َ َ َ ُ َ َ َّ
٢٣ ليِدبت اولدب امو ۖرِظتني نم
Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na
Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea,
wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo. (Al-Ahzaab, 33:23)
Miongoni mwa Waumini wapo watu waliomuahidi Allah (S.W) kuwa watasimama
imara na Mtume katika vita. Nao wakatimiza ahadi yao. Miongoni mwao wapo walio
pata utukufu wa kufa mashahidi, na wengine wamebakia hai wakingojea nao kupata
utukufu huo. Wala hawakuigeuza ahadi ya Allah (S.W) waliyoiweka juu ya nafsi zao,
wala hawakugeuza chochote katika hayo. Kufanana kwao, Ahadi ya Waumini kwa Allah
(S.W), inafanana na Ahadi ya Utii katika lengo kwani suala la kupambana katika njia ya
Allah (S.W) ni sehemu ya utii walioahidi wanadamu kuutekeleza katika Ahadi ya Utii.
Kutofautiana kwao, katika wahusika, Ahadi ya Waumini kwa Allah (S.W), inawahusu
Waislamu tu wakati Ahadi ya Utii inawahusu wanadamu wote.
Mazingatio kutokana na ahadi ya utii
Ahadi ya Utii inaoneshwa kwamba mwanadamu alimuahidi Allah (S.W) kumwabudu
Yeye pekee kama Mola wake Mlezi. Ili mtu asisahau ahadi yake, Allah (S.W) ametuma
Manabii kwa mwanadamu:
ۡ َّ ُ ۡ َ َ ُ َّ ْ ُ َ ۡ َ َ َّ ْ ُ ُ ۡ َ ً ُ َّ َّ ُ ّ ُ َ ۡ َ َ ۡ َ َ َ
ٰ
نم مهنِمف ۖتوغطلٱ اوبِنتجٱو للٱ اودبعٱ نأ لوسر ٖةمأ ك ِ ف انثعب دقلو
ِ
ِ
َ
َ ۡ َ ْ ُ ُ َ َ ۡ ْ ُ َ ُ َ َ َّ ۡ َ ۡ َّ َ ۡ َّ ُ ۡ َ ُ َّ َ َ
ٰ
فيك اورظنٱف ِ ضرۡلٱ ِ ف اويرِسف ۚةللضلٱ ِهيلع تقح نم مهنِمو للٱ ىده
َ ّ َ ۡ ُ َ َ َ َ
ُ
ٰ
.٣٦ ينبِذكملٱ ةبِقع نك
ِ
Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume tukasema kwamba:
Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao
wapo alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao ulio
wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje
mwisho wa wanao kanusha.(An-Nahl 16:36)
235