Page 244 - EDK_F5
P. 244
SURA YA TISA HISTORIA KATIKA UISLAMU
Kwanza, Ahadi ya Amana. Ahadi ya Amana inauhusiano wa karibu na Ahadi ya Utii.
Hii ni kwa sababu zote zinamkusudia mwanadamu kutimiza lengo la kuumbwa kwake
ambalo ni kumwabudu Mola wake Mlezi. Katika kujadili hili, aya ya Qur’an, (Ahazab,
33:72) inasema:
ۡ
FOR ONLINE READING ONLY
َ ۡ َ ۡ َ َ َ َ ۡ َ َ َ ۡ َ َ َ َ ۡ َ َ ۡ َ َ َ َّ َ َ َ َ َ َ ۡ َ ۡ َ َّ
َ
ٰ ٰ
نقفشأو اهنلِمي نأ ينبأف ِ لابلٱو ِ ضرۡلٱو ِ تومسلٱ ع ةناملٱ انضرع انِإ
ِ
ٗ ُ َ ٗ ُ َ َ َ ُ َّ ُ َ ۡ َ َ َ َ َ ۡ
َ
ٰ
.٧٢ لوهج امولظ نك ۥهنِإ ۖنسنلٱ اهلحو اهنِم
ِ
Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu na ardhi na milima;
na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanadamu
akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhalimu mjinga. (Al-Ahzab, 33:72)
Yaani, Sisi kwa hakika tulizitaka mbingu na ardhi na milima zichukue amana, nazo
zikakataa kuichukua, na wakaiogopa. Lakini mwanadamu aliichukua. Hakika yeye
amekuwa ni mkubwa wa kujidhulumu nafsi yake kwa kutojua jukumu la kuchukua huko.
Kufanana kwao, lengo la Ahadi ya Amana linafanana na la Ahadi ya Utii kwani zote
zinakusudia kumfanya mwanadamu atekeleze lengo la kuumbwa kwake, ambalo ni ibada
(Ad-Dhariyat, 51:56). Kutofautiana kwao, tofauti zake ni mbili; mosi, Ahadi ya Utii
ilihusisha mwanadamu na Mola wake tu, wakati Ahadi ya Amana ilihusisha mbingu,
ardhi, milima na mwanadamu pamoja na Mola wao Mlezi. Pili, maazimio ya Ahadi ya Utii
yalikuwa ni kwamba mwanadamu kumtii Mola wake Mlezi na Mola Mlezi kumruzuku
mwanadamu. Wakati maazimio ya Ahadi ya Amana yalikuwa ni mwanadamu kuibeba
amana na huku viumbe vitamtumikia mwanadamu katika kutekeleza ubebaji wa amana
aliyoikubali kuibeba.
Pili, ahadi ya mitume. Hii ni ahadi iliyofungwa baina ya Allah (S.W) na Mitume wake
wote kwa wanadamu. Allah (S.W) aliifanya ahadi hii kwa Mitume wote, waliotajwa na
ambao hawajatajwa katika Qur’an. Kuanzia Nabii Adam mpaka Mtume Muhammad
(S.A.W). (33:7,23)
ۡ َ َ ٰ َ ُ َ َ َ ۡ ُّ َ َ َ ۡ ُ َ َ َ ّ َّ َ َ ۡ َ َ ۡ
ٰ
نبٱ سيِعو سومو ميِهٰربوَإِ ٖ حون نِمو كنِمو مهقثيِم نۧـيبلنٱ نِم انذخأ ذوَإِ
ِ ِ
ِ
َ
ٗ َ ً َ ّ ُ ۡ َ ۡ َ َ َ َ ۡ َ
ٰ
.٧ اظيِلغ اقثيِم مهنِم انذخأو ۖميرم
Na tulipo chukua ahadi kwa Manabii na kwako wewe, na Nuhu na
Ibrahim na Isa mwana wa Mariamu, na tulichukua kwao ahadi ngumu.
(Al-Ahzab, 33:7, 23)
Yaani, kumbusha pale tulipowekeana ahadi na Manabii wote waliotangulia kuwa
watafikisha ujumbe na kulingania Dini iliyo sawa, na wewe (Muhammad), na Nuhu,
Ibrahim, Musa, na Isa bin Maryamu; na tukachukua kwao ahadi yenye shani kubwa.
234