Page 282 - EDK_F5
P. 282
SURA YA KUMI HISTORIA YA UISLAMU
Mtume Muhammad (S.A.W) baada tu alipopewa utume, alitakiwa kuufikisha ujumbe
huo kwa kuanza na waliomzunguka kisha auwasilishe kwa ulimwengu mzima. Naye
hakufanya ajizi, kwani hakupumzika wala kutumia muda mwingi na watu wake wa
nyumbani. Alisimama wakati wote akiwalingania watu juu ya Allah (S.W). Aliubeba
mzigo huo mzito mabegani mwake, na wala hakuutua, pamoja na kuwa ulikuwa ni mzito.
FOR ONLINE READING ONLY
Mzigo wa kuwaongoza walimwengu wote, katika hali zote; amani na hofu, raha na karaha
kwa miaka ishirini na tatu.
Mchakato wa ulinganiaji wakati wa Mtume Muhammad (S.A.W) umegawika katika
vipindi viwili: Kipindi cha Makka, kilichochukua miaka kumi na tatu na Kipindi cha
Madina, kilichochukua miaka kumi. Kila kimoja kati ya vipindi hivyo, kilikusanya awamu
tatu; kila awamu ilikuwa na mambo yaliyokuwa tofauti na awamu nyingine. Kwanza,
kipindi cha Makka kilikuwa na; (i) Awamu ya da’awa ya siri, ilidumu katika miaka mitatu
ya mwanzo ya utume. (ii) Awamu ya da’awa kwa watu wa Makka iliyoanza mwaka wa
nne mpaka mwaka wa kumi wa utume. (iii) Awamu ya da’awa nje ya Makka, iliyoanza
mwishoni mwa mwaka wa kumi wa utume mpaka kabla ya Hijra ya Madina. Pili, kipindi
cha Madina nacho kilikuwa na awamu tatu; (i) Awamu ya kustawisha hali za Waislamu
na miundombinu ya Madina, hii ilihusisha miaka ya mwanzo ya Hijra (ii) Awamu ya
kupambana na udhalimu wa washirikina wa Makka, Wayahudi na Wanafiki wa Madina.
(iii) Awamu ya kupambana na udhalimu wa dola za Kirumi na Kiajemi, hii ilianza mwaka
wa saba hadi Mtume Muhammad (S.A.W) alipotawafu.
Njia alizotumia Mtume Muhammad (S A W) Kulingania Uislamu na
Hekima Zake
Kazi ya 10 6
Shirikiana na wanafunzi wenzako kusoma aya na tafsiri yake, kisha bainisha mambo
makubwa manne yanayotajwa katika aya hiyo
َ
َ ْ َ ْ ُّ َ ْ َ ْ ْ َ َ َ ًّ َ َ ْ ُ َ ْ َ ْ ُ َ ْ َّ َ َ ْ َ َ َ
كِلوح نِم اوضفنل بلقلا ظيِلغ اظف تنك ولو ۖ مهل ت ِ لن ِللا نِم ٍةحر امبف
ِ
ِ
َ
َّ َّ َ َ ْ َّ َ َ ْ َ َ َ َ ْ َ ْ ْ ُ ْ َ ْ ُ ْ ْ َ ْ َ ْ ُ ْ َ ُ ْ َ
َ َ
َ
نِإ ۚ ِللا ع كوتف تمزع اذإف ۖ رملا ِ ف مهرواشو مهل رِفغتساو مهنع فعاف ۖ
ِ
ِ
ِ
َ ّ َ َ ُ ْ ُّ ُ َّ
َ
١٥٩ ينِ ِ كوتملا بِي للا
Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio
umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo
mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia. Basi wasamehe, na waombee
maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi
mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda
wanaomtegemea. (Al-Imran, 3:159).
272