Page 284 - EDK_F5
P. 284
SURA YA KUMI HISTORIA YA UISLAMU
e) Kuchukia maovu na kujitenga pangoni katika pango la Hira ili kutafuta msaada wa
Allah (S.W) wa namna ya kuikomboa jamii kutokana na dhulma.
Aidha, Mtume Muhammad (S.A.W) alipewa mafunzo mahususi kupitia Qur’an kama
ifuatavyo:
FOR ONLINE READING ONLY
a) Ambapo katika wahyi wa kwanza; aliamrishwa asome kwa ajili ya Mola wake
(‘Alaq, 96:1-5) na wahyi uliofuatia unaopatikana katika suratul Muzzamil,
Muddathir na Qalam Mtume Muhammad (S.A.W) aliamrishwa kuswali usiku,
kusoma Qur’an kwa mazingatio, kumtaja Allah (S.W) kila wakati na kunyenyekea
kwake, kumtegemea Allah (S.W), kuwa na subira, kusafisha nguo, kupuuza mabaya,
kufanya ihsan kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (S.W)- Rejea Muzzammil, 73:1-
10) na (Muddathir,74:1-7).
Maandalizi haya yalimfanya awe na tabia njema kiasi cha kuweza kumvutia mtu yeyote
aliyekutana naye. Allah (S.W) anampongeza kupitia Qur’an kwa kusema: “Na hakika
wewe una tabia tukufu.” (Qalam, 68:4).
Kuwaunganisha Answari na Muhajirina, Muhajirina walikuwa pamoja na Mtume
Muhammad (S.A.W) kwa muda wa miaka kumi na tatu, hivyo, walikuwa wamepata
mafundisho ya kutosha kuhusu Uislamu, wakati Answari walikuwa wapya katika
Uislamu. Hivyo, Mtume Muhammad (S.A.W) alitumia fursa hiyo kuwaunganisha baina
ya makundi hayo mawili ili Muhajirina wawasomeshe Answari mambo yanayohusiana
na Uislamu wao. Aidha, aliwaunganisha mtu mmoja kutoka Answari na mmoja kutoka
Muhajirina na kuwafanya kuwa ndugu wa kiimani baina yao. Lengo ni kufuatiliana kwa
ukaribu ili kila mmoja anufaike na neema alizokuwa nazo ndugu yake, ikiwemo elimu na
mali. Udugu huo ulifanywa kama wa damu. Ikawa kuko kurithiana baina yao kwa sudus
(1/6), mpaka ilipokuja kufutwa sharia hii.
َ
ۡ
َ
ۡ ُ ُ َ ۡ ُ ُ َ ۡ ۡ َ َ َ َ َّ َ َ ُ َ ۡ َ ۡ َ َ َ ۡ َ َ َ َّ َ َ َ َ َ َ ّ ُ َ
ٰ
ٰ
ٰ
مهوتأـف مكنميأ تدقع نيِلٱو ۚنوبرقلٱو نا ِ لدولٱ كرت امِم لوم انلعج كِلو
ِ
ِ
ٖ
ً َ ۡ َ ّ ُ َ ٰ َ َ َ َ َّ َّ ۡ ُ َ َ
.٣٣ اديهش ٖءش ك ع نك للٱ نِإ ۚمهبي ِ صن
ِ
ِ
Na kila mmoja tumemwekea warithi katika waliyoyaacha wazazi wawili
na jamaa. Na mlio fungamana nao ahadi wapeni fungu lao. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu, (Nisaa, 4:33).
Mfano mzuri wa kuunganishwa watu wawili wawili baina ya Answari na Muhajirina ni
Abdur Rahman bin Auf aliyekuwa muhajiri aliyefanywa kuwa ndugu wa Saad aliyekuwa
274