Page 283 - EDK_F5
P. 283
SURA YA KUMI HISTORIA YA UISLAMU
Mtume Muhammad (S.A.W) alitumia njia mbalimbali za kufikisha ujumbe ili kufanikisha
lengo la kutumwa kwake kwa walimwengu, miongoni mwa njia hizo ni:
Kulingania kwa siri: njia hii ndio msingi wa ulinganiaji wa Mtume Muhammad (S.A.W),
alianza kulingania familia yake, kisha rafiki zake na jamaa zake wa karibu. Alikuwa
FOR ONLINE READING ONLY
anakutana nao kwa siri mmoja mmoja; kwa njia hii walisilimu watu kama Abubakar
(R.A) aliyekuwa rafiki yake, Ali bin Abi Talib (R.A) mtoto wa ami yake, Khadija binti
Khuwailid (R.A) mke wake na Zaid bin Harith (R.A) mtumishi wake wa ndani. Hao
ni watu wa mwanzo kusilimu, waliokuwa karibu mno na Mtume Muhammad (S.A.W).
Pia, aliendelea kutumia njia hii ya siri na kufanikiwa kupata kundi la watu zaidi ya 40
na kuamua kuwapa mafunzo kuhusu Uislamu katika nyumba ya Bwana Arqam bin Abi
Arqam.
Kutoa hotuba hadharani: Mtume Muhammad (S.A.W) alipoamrishwa na Mola wake
atangaze ujumbe wa Uislamu kwa jamii nzima kupitia Qur’an (Hijri, 15:94 na Shuaraa,
26:214-217) alipanda juu ya mlima Safa akapiga mbiu ya dharura, kuziita koo zote za
Kiqureshi kwa majina yao. Baadaye, akatoa hotuba na kueleza lengo la kutumwa kwake
kwa walimwengu, ingawa hawakumkubali na Abu Lahab akamuapiza, ndio Allah (S.W)
akamlani kama ilivyobainisha katika Qur’an (Surat Lahab, 111:1-3).
Kuishi kwa tabia njema, Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa hana mpinzani kwa
tabia njema katika maisha yake. Alikuwa na tabia zilizomvutia kila aliyeamiliana naye.
Hii ilitokana na maandalizi aliyoyapata kabla na wakati wa kupewa utume. Mtume
Muhammad (S.A.W) aliandaliwa bila ya kujijua kabla ya kupewa utume, maandalizi haya
yanajulikana kama maandalizi ya Ki-ilham; miongoni mwa maandalizi hayo ni:
a) Kuzaliwa katika kabila la Qureysh katika kizazi cha Nabii Ibrahim (A.S) kupitia
kwa Nabii Ismail (A.S);
b) Kupewa jina la Muhammad lenye maana sawa na jina la Ahmad lililotabiriwa
katika Injili;
c) Malezi bora aliyoyapata kutoka kwa mama yake mzazi Amina, mama yake wa
kunyonya Halima, babu yake Abdul-Muttalib na ami yake Abu Talib;
d) Ndoa ya Mtume Muhammad (S.A.W) na Bi Khadija (R.A) ilikuwa ni mpango wa
Allah (S.W) ili kumtajirisha Mtume Muhammad (S.A.W) kupitia mkewe huyo,
baadaye mali yake ikatumikia jamii ya Kiislamu; na
273