Page 286 - EDK_F5
P. 286
SURA YA KUMI HISTORIA YA UISLAMU
َ
َ ۡ َ ۡ ْ ُّ َ َ ۡ ۡ َ َ َ ًّ َ َ ُ َ ۡ َ ۡ ُ َ َّ َ ّ َ ۡ َ َ َ
ۖكِلوح نِم اوضفنل بلقلٱ ظيِلغ اظف تنك ولو ۖمهل ت ِ لن ِللٱ نِم ٖةحر امبف
ِ
ِ
َ
َّ َّ َ َ ۡ َّ َ َ ۡ َ َ َ َ ۡ َ ۡ ۡ ُ ۡ َ َ ۡ ُ ۡ ۡ َ ۡ َ ۡ ُ ۡ َ ُ ۡ َ
َ َ
نِإ ِۚللٱ ع كوتف تمزع اذإف رملٱ ِ ف مهرواشو مهل رِفغتسٱو مهنع فعٱف
ِ
ِ ِۖ
َ ّ َ َ ُ ۡ ُّ ُ َّ
َ
.١٥٩ ينِ ِ كوتملٱ بِي للٱ
FOR ONLINE READING ONLY
Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio
umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu,
bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira,
na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee
Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao
mtegemea, (Al-Imran, 3:159).
Kutatua changamoto za jamii, Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa hajisikii vyema
kama kuna mtu yeyote katika wafuasi wake au jamii kwa ujumla anasumbuka na tatizo,
alililazimisha kumsaidia au kuwa sababu ya kulitatua tatizo lile. Qur’an inaweka bayana
hilo kwa kusema:
َ
َ
ٓ
ُ ۡ َ ٌ َ ۡ ُّ َ َ ۡ َ ٌ َ ۡ ُ ُ َ ۡ ّ ٞ ُ َ ۡ ُ َ َ ۡ َ َ
مكيلع صيرح متِنع ام ِهيلع زيزع مكِسفنأ نِم لوسر مكءاج دقل
ِ
ِ
ٞ َّ ٞ ُ َ َ ۡ ُ ۡ
.١٢٨ ميِحر فوءر ينِنِمؤملٱب ِ
Hakika amekwishakujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe;
yanamhuzunisha yanayokutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa
Waumini ni mpole na mwenye huruma. (Taubah,9:128).
Kubashiri na kuonya: Hii ni njia waliyoitumia Mitume wote kwani ndio lengo hasa
la kuletwa Mitume duniani. Mtume Muhammad (S.A.W) mara kwa mara aliwabashiria
Maswahaba zake mambo mazuri kama vile waliotenda mema kwa kiwango cha juu
aliwabashiria Pepo, mfano mzuri ni Maswahaba kumi waliobashiriwa Pepo. Aidha,
alionya tabia mbaya kwani matokeo yake ni Motoni. Qur’an inathibitisha hili kwa kusema:
ۡ
ٗ َ َ ٗ ّ َ ُ َّ َ َ َ ۡ َ ٓ َ َ َ َ ّ َ ۡ َ ُ َ َ ۡ َ ّ َ ۡ َ
َ
ٰ
ٰ
.١٠٥ اريِذنو ا ِ شبم لِإ كنلسرأ امو ۗلزن قلٱبو هنلزنأ قلٱبو
ِ
ِ
ِ
ِ
Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma
ila uwe mbashiri na mwonyaji. (Israa, 17:105).
Kuwa mfano mwema wa kuigwa: Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa mfano wa
kuigwa katika kila kipengele cha maisha yake. Hii ni kwa sababu alivaa kofia za watu
wote mbele ya macho ya Maswahaba wake. Alikuwa mwalimu kwani aliwafunza, alikuwa
daktari kwani aliwatibu, alikuwa askari kwani alisimamia sheria katika kulinda uhai na
mali zao, alikuwa mshauri kwani aliwapa ushauri nasaha, alikuwa mlezi kwani aliwalea,
276