Page 285 - EDK_F5
P. 285
SURA YA KUMI HISTORIA YA UISLAMU
Answari. Pia, Salman Faris aliyechukuliwa kama muhajiri kwa kuwa hakuwa na asili ya
Madina wala Makka, aliunganishwa udugu na Abu Dardaa aliyekuwa Answari. Hawa na
wengine walitumia muda mwingi kuelemishana kuhusu dini yao na kusaidiana katika
maisha yao yote.
FOR ONLINE READING ONLY
Kufunga mikataba: mikataba iliwezesha kufikisha ujumbe wa Uislamu wakati wa
Mtume Muhammad (S.A.W) kwani ilisaidia uhusiano mzuri baina ya waumini wao
kwa wao na hata wao na wasiokuwa Waislamu. Mfano wa mikataba iliyotumika katika
kulingania ni Mikataba miwili ya Aqaba, Mkataba wa Hudaibiya, na Mkataba wa Madina.
Kupitia mikataba hii watu walisilimu na wengine kuona uzuri wa Uislamu. Mfano, Qur’an
inasimulia vipengele vya mkataba wa wanawake walio hajir kwenda Madina.
َ
َ َ ٗ ۡ َ َّ َ ۡ ۡ ُ َّ َ َ َ َ َ ۡ َ ُ ُ َ ۡ ُ ۡ َ َ َ َ َّ َ ُّ َ
ٓ
ٰٓ
ُّ
ٰ
ٰٓ
لو أـيش ِللٱب نكشي ل نأ ع كنعيابي تنِمؤملٱ كءاج اذِإ بلنٱ اهيأي
ِ
ِ
ِ
ِ
َ
َ
ۡ
َ
َّ ۡ َ ۡ َ ُ َ َ ۡ َ َ ۡ ُ َ ۡ َ َ َ َّ ُ َ ۡ َ ُ ۡ َ َ َ َ ۡ َ َ َ َ ۡ ۡ َ
ٰ
ٰ
نهيِديأ ينب ۥهنيتفي نتهبب ينِتأي لو نهدلوأ نلتقي لو ينِنزي لو نقسي
ِ
ِ
ِ
ِ
ٖ
َ
ٞ ُ َ َ َّ َّ َ َّ َّ ُ ۡ ۡ َ ۡ َ َّ ُ ۡ َ َ ُ ۡ َ َ َ ۡ َ َ َ َّ ُ ۡ َ َ
روفغ للٱ نِإ ۚللٱ نهل رِفغتسٱو نهعيابف ٖ فورعم ِ ف كني ِ صعي لو نهِلجرأو
ِ
ِ
ٞ َّ
.١٢ ميِحر
Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba
hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba,
wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta
uzushi wanao uzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala
hawatakuasi katika jambo jema, basi peana nao ahadi, na uwatakie
maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi
maghfira, Mwenye kurehemu, (Mumtahina, 60:12).
Kuwa mpole kwa wafuasi wake: Mtume Muhammad (S.A.W) hakuishi kwa ukali na
wafuasi wake, hata iweje aliwavumilia na kuwachukulia mapungufu yao ya kibinadamu.
Mfano, katika vita vya Uhud kuna Maswahaba 50 waliowekwa katika mlima na kupewa
amri ya kutoshuka, ila kwa amri nyingine ya Mtume Muhammad (S.A.W), lakini wao
walishuka, walipoona Waislamu wanakaribia kushinda. Hapo ushindi ukabadilika,
kutoka kwa Waislamu ukenda kwa Washirikina, Waislamu 70 wakafa shahidi, Mtume
Muhammad (S.A.W) akajeruhiwa meno yake, lakini yeye hakuwakaripia, aliwasamehe
na kuwaombea msamaha kwa Allah (S.W). Jambo hili liliwafanya watu wanaosilimu
kutotamani kutoka katika Uislamu. Qur’an inasimulia tukio hili:
275