Page 150 - SayansiStd4
P. 150
13. Cheza mchezo wakati namba katika chumba cha kwanza
ni 10 na chumba cha pili namba ikiwa ni 6. Hii ni hali ya
kweli kwa sababu 10 ni kubwa kuliko 6. Je, nini umesikia
katika hatua hii?
FOR ONLINE READING ONLY
14. Badilisha namba ili chumba cha kwanza iwepo namba 6
na chumba cha pili iwepo namba 10. Kisha, cheza tena
mchezo. Hii si hali ya kweli kwa sababu 6 si kubwa kuliko
10. Je, umesikia nini katika hatua hii?
Kazi ya kufanya namba 14: Kuunda mchezo wa kumfanya
aende juu na chini ‘Sprite’(Cat) huku akitoa sauti
Hatua zifuatazo zitakuongoza kuunda mchezo ambapo
mchezaji atampeleka ‘Sprite’ kwenda juu ama chini. Wakati
huo huo Sprite atakuwa anatoa sauti.
1. Bofya menyu ya bloku za ‘Matukio’.
2. Buruta na dondosha bloku ya ‘wakati kitufe cha
kinapobonyezwa’ kwenye eneo la kuandikia kama
inavyoonekana katika Kielelezo namba 42. Kisha
changua ‘kishale juu’.
Kielelezo namba 42: Kuchagua ‘kishale juu’
143
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 143
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 143 14/01/2025 18:39