Page 169 - SayansiStd4
P. 169
12. (a) Andaa programu itakayomwezesha Sprite kwenda
mahali popote kwa kutumia opereta ya kubwa kuliko.
Ingiza namba 8 katika chumba cha kwanza na 5 katika
chumba cha pili. Kisha, jaribu kucheza mchezo wako. Nini
FOR ONLINE READING ONLY
kimetokea baada ya kujaribu?
Rudia sehemu 12(a), kwa kuingiza namba 9 katika chumba
cha kwanza na namba 13 katika chumba cha pili. Nini
kimetokea?
13. Chora umbo la mstatili. kisha likae juu ya maduara
mawili yanayolingana ukubwa. Duara moja liwe upande
wa kushoto na jingine liwe upande wa kulia. Paka rangi
michoro yako.
Msamiati
Buruta kuchagua na kuelekeza upande husika
Kiolesura ni neno linalotumika kuelezea njia inayowezesha
mawasiliano kati ya binadamu na kompyuta au
kifaa kingine cha kielektroniki
Mantiki kufanya jambo kwa njia ya utaratibu unaoonesha
sababu zilizo wazi na zinazofaa zilizopelekea
kufikia hitimisho
Mlolongo mpangilio maalum unaowezesha vitu
vinavyohusiana kuwa na mfuatano wenye
utaratibu
162
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 162
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 162 14/01/2025 18:39