Page 16 - EDK_F5
P. 16
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
kuwaonesha watu jinsi ya kuishi maisha yanayomridhisha Allah (S.W). Mafanikio ya
mwanadamu yanaweza kuhakikishwa pale tu anapofuata kitabu kutoka kwa Allah (S.W)
na kufuata Sunnah za Mtume Muhammad (S.A.W).
Tatu, Akhera, binadamu sio wa milele. Wanadamu wote watakufa na watahudhurishwa
FOR ONLINE READING ONLY
mbele ya Mola wao Mlezi. Watalazimika kuwajibika kwa matendo yao katika maisha
haya. Kila mtu atalipwa kwa kuneemeshwa au kuadhibiwa, kulingana na jinsi alivyofanya.
Ikiwa alitii katika maisha ya hapa duniani, akhera ataneemeshwa lakini ikiwa ameasi basi
na huko ataadhibiwa, hakuna namna ya tatu.
Nne, Ukhalifa, dunia ni sehemu ndogo ya ulimwengu. Wanadamu wameteuliwa
kuwa makhalifa wa Allah (S.W) duniani. Yaani, amekusudiwa kuimarisha dunia kwa
miundombinu na mazingira kuwa rafiki, kuamrisha mema na kukataza mabaya pamoja na
kuweka utawala wa sharia, ili haki itendeke kwa kuheshimiana, kusaidiana, kuhurumiana,
kuungana mkono na kusameheana. Ni wajibu kwa khalifa huyo kuhakikisha Ufalme wa
Allah (S.W) unatawala katika dunia kama unavyotawala mbinguni.
Tano, Umoja wa wanadamu, wanadamu wote wametokana na Adam na Hawa, hivyo
wote ni sawa na ndugu. Tofauti zote zitokanazo na rangi, kabila, tabaka na kadhalika ni
kwa ajili ya kujuana tu imekatazwa kuzidumisha. Mwarabu hana ubora hata kidogo juu
ya asiye Mwarabu, mweupe kwa mweusi, tajiri kwa maskini, kiongozi na anayeongozwa.
Anayeheshimika zaidi mbele ya Uislamu ni yule ambaye ni mchamungu zaidi.
Sita, Uhuru, kila mtu, awe mdogo au mkubwa, tajiri au masikini, mwanamume au
mwanamke, mwajiri au mwajiriwa, wote ni watumwa wa Allah (S.W), na wana wajibu wa
kufuata amri zake. Licha ya kuwajibika kumtii Mola wake Mlezi, mwanadamu amepewa
uhuru wa kuchagua; amtii au amuasi. Lakini aelewe kwamba hakuna malipo kwa mtenda
mazuri, ila kulipwa mazuri na kinyume chake kwa mtenda mabaya. Aidha, miongoni
mwa wanadamu, wenyewe kwa wenyewe kila mtu ana uhuru sawa na mwingine. Kila
mwanamume au mwanamke amezaliwa kutoka tumboni mwa mama yake akiwa huru.
Hakuna mtu aliye na haki ya kuzuia uhuru wa wengine au kujaribu kuwafanya wengine
watumwa na kuwalazimisha kufuata amri zake.
Saba, Imani, hakuna kizuizi kwa dhamira, maoni na mtazamo. Kila mtu ana uhuru kamili
wa imani au dini. Imani yoyote au mfumo wa imani mtu anaotaka kuufuata unaweza
kuufuata, ingawa Uislamu unabaki kuwa ndio imani, mfumo au njia bora zaidi kwa
wanadamu, kwani ndio mfumo wa maisha uliowekwa na Allah (S.W).
Nane, Sharia, kila mtu yuko chini ya sharia ya Allah (S.W). Hakuna aliyekuwa na haki ya
kuikiuka au kuitunga yake au kuzifuata za watu ikiwa zinakiuka sharia hiyo. Sharia hiyo,
6