Page 15 - EDK_F5
P. 15
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
Malengo ya elimu katika mfumo wa kibepari
Kwa vile kufanikiwa au kushindwa kwa mfumo wa ubepari kunatokana na sifa za
wananchi wake, kwa hiyo lengo la msingi la elimu mbele ya watetezi wa ubepari
ni kuwafanya raia kuwa wema kwa taifa. Hata hivyo, huyapa umuhimu usiofaa
FOR ONLINE READING ONLY
maendeleo ya mali na mafanikio ya kifedha. Kuna mapambano ya kuendelea
miongoni mwa raia wake ili kuwatangulia wengine katika masuala ya utajiri. Pia
katika mfumo huu, maadili hupoteza thamani yake, kwani hayana thamani ya
kudumu. Wakati wowote kunapotokea mgongano wa maslahi kati ya serikali na
maadili, wananchi hufundishwa kuacha maadili.
Madhara ya mfumo wa elimu wa kibepari
Kwa kuwa ubepari, huyapa umuhimu usiofaa maendeleo ya mali na mafanikio ya kifedha,
kuna mapambano ya kuendelea miongoni mwa raia wake ili kuwatangulia wengine katika
masuala ya utajiri. Kwa hiyo, utoaji wa elimu kupitia misingi ya kibepari, taasisi za elimu
zinajikuta zinazalisha wahitimu wasio na maadili. Wahitimu wasiojali utu, uzalendo wa
uadilifu katika kuhakikisha maslahi ya jamii kwa ujumla.
Mfumo wa elimu katika Uislamu
Kazi ya 1 2
Shirikiana na wanafunzi wenzako kujadili maana na malengo ya elimu kwa mujibu
wa Uislamu
Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, yaani haujaacha nyanja wala kipengele chochote
cha maisha isipokuwa umekiweka bayana. Hii ndiyo dini pekee ya kweli na sahihi kwa
wanadamu wote. Allah (S.W) amebainisha wazi kwamba mafanikio ya maisha haya na
maisha ya akhera yanaweza kupatikana tu kwa kuikubali na kuifuata dini ya Uislamu.
Kwa hiyo, mfumo wa elimu katika Uislamu umejengwa juu ya misingi mikuu minane
ifuatayo:
Mosi, Mungu mmoja, Allah (S.W) pekee ndiye Muumba, Mmiliki na Mtawala wa
ulimwengu mzima. Wanadamu wote ni watumwa Wake na Yeye pekee ndiye anayestahiki
kuwa Mfalme na Mwenye enzi. Kila mwanadamu lazima ahakikishe anabaki kuwa
mtumwa Wake na kumuabudu Yeye pekee.
Pili, Utume, Allah (S.W) aliwatuma Mitume wake kwa wanadamu kwa ajili ya uongofu
wao. Mitume na Manabii, walileta amri zake kupitia vitabu mbalimbali. Mtume Muhammad
(S.A.W) ndiye mjumbe wa mwisho wa Allah (S.W). Aliteremshiwa Qur’an ili aitumie
5