Page 10 - EDK_F5
P. 10
DIBAJI
Aidha, kuna vipengele vipya ambavyo havikuwahi kufundishwa katika Sekondari ya
chini kama vile:
(a) Mchango wa Waislamu katikaTaaluma; katika sura ya kwanza;
(b) Vitimbi vya wapinzani dhidi ya Qur’an na athari zake; katika sura ya nne;
FOR ONLINE READING ONLY
(c) Kufasiri Qur’an; katika sura ya tano;
(d) Hoja potofu zinazonasibishwa na Sunnah; katika sura ya sita; na
(e) Ahadi ya Utii; katika sura ya tisa.
Kwa ujumla, kitabu kinamuandaa mhitimu atakayemudu kuamiliana na jamii yenye
imani, itikadi, maadili na mitazamo tofauti, atakayekuwa raia wa kimataifa, msomi
nyumbufu, mbunifu, msuluhishi na mtatuzi wa changamoto zinazomkabili mwanadamu
na ulimwengu wake. Ingawa, tukiri kuwa kwa vile ni kitabu kilichoandikwa na wanadamu,
hakikosi kuwa na dosari za hapa na pale, hivyo wasomaji wawe huru kuwasilisha maoni
yao TISTA, kwa ajili ya marekebisho kwa matoleo yajayo.
Jumuiya ya Ufundishaji wa Masomo ya Kiislamu Tanzania (TISTA)
viii