Page 14 - EDK_F5
P. 14
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
Mfumo wa elimu wa ujamaa
Ujamaa ni mfumo uliojikita katika ulimwengu wa kimaada au kupenda mali na kupiga
vita dini na maadili. Mfumo huu unapambana na matabaka kwa manufaa yake. Katika
Ujamaa, watu na ubinafsi wao hauna thamani yoyote. Maisha ya raia na heshima yao iko
FOR ONLINE READING ONLY
chini ya serikali, ambayo pia inamiliki rasilimali zote za nchi.
Lengo la elimu katika Ujamaa ni kuwawezesha wanadamu kuwa watumishi wasio na
ubinafsi na wenye kujali maslahi ya jamii. Hufundishwa umuhimu wa kujenga uchumi
wa pamoja badala ya uchumi binafsi. Pia, hujengwa kitabia kuchukia masuala ya dini na
kupiga vita uwepo wa Allah (S.W).
Madhara ya mfumo wa elimu wa ujamaa
Mfumo wa elimu wa kijamaa una madhara yafuatayo:
Kupinga uwepo wa Allah (S W), kunawafanya raia kutokuwa na uadilifu na kukosa
maadili, hutokea uharibifu wa maadili katika jamii. Hujidhulumu wenyewe na
kuwadhulumu wengine. Wakati wowote wanapopata fursa hawafikirii mara mbili, iwe
kuna madhara au hakuna.
Utu wa mtu binafsi umeharibiwa, Mtu amepewa akili na vipawa vingine ili vimsaidie
kuishi kwa uhuru na aweze kuwasaidia wengine, kwa kukosesha uhuru binafsi kinachotokea
ni kuidumaza akili na vipawa vyake.
Wanafunzi huwa katika vita endelevu dhidi ya tamaa, maoni na dhamira zao.
Wanakuwa na huzuni na msongo wa mawazo, kutokana na kutumikia nguvu za nje kwa
lazima. Hakuna shaka kwamba wanafunzi kama hao hawawezi kamwe kuwa na utu au
tabia za kimaadili.
Uzalishaji mali umepewa nafasi ya kupitiliza, ujamaa umewafanya watu kama
wanyama, kupitia mfumo wa elimu katika suala la uchumi, mtu anapaswa kuzalisha mali
tu bila ya kuzingatia mambo ya kimaadili. Kwa hivyo, jambo muhimu kwao ni mtu kupata
riziki na sio kitu kingine chochote.
Watu wote wa taifa, isipokuwa wachache waliochaguliwa, wamegandishwa kisaikolojia.
Watu wamenyimwa amani na utulivu wa dunia na maisha ya akhera. Hii ni kwa sababu
saikolojia ya watu wa taifa la kijamaa inawaza kazi tu, akili haina muda wa kupumua au
kufikiria mambo mengine, kama kutafakari kuhusu dunia na mustakabali na maisha ya
akhera.
4