Page 13 - EDK_F5
P. 13
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
asiyetofautiana na asiyesoma katika kutekeleza majukumu ya maisha, hatofautiani na
punda aliyebeba mzigo wa vitabu asivyofaidika navyo. Mfano huu umebainishwa katika
Qur’an kama ifuatavyo:
ُ َ َ َ ۡ ۢ َ َ ۡ َ ُ ۡ َ َ ۡ َ َ َ َ ُ ۡ َ َ ُ َ ٰ َ ۡ َّ ْ ُ ّ ُ َ َّ ُ َ َ
ۡ َّ
لثم سئب ۚارافسأ لِمي رامِلٱ لثمك اهولِمي مل مث ةىرولتٱ اولِح نيِلٱ لثم
ِ
ِ
ِ
FOR ONLINE READING ONLY
ُ
َ َّ َ ۡ َ ۡ ۡ َ َ ُ َّ َ َّ َ ْ َّ َ َ َّ ۡ َ ۡ
ٰ
ٰ
٥ينِمِلظلٱ موقلٱ يِدهي ل للٱو ِۚللٱ ِ تيأَ ب اوبذك نيِلٱ ِموقلٱ
ِ
Mfano wa wale waliopewa Taurati kisha hawakuichukua (kwa kuitumia)
ni kama punda anayebeba vitabu vikubwa vikubwa (bila ya kufaidika
kwavyo). Ni mbaya kabisa mfano wa watu waliokadhibisha aya za
Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu”
(Al-Jumu’a, 62:5).
Kwa mantiki hiyo, haitarajiwi kumuona Muislamu, anayejua madhara ya pombe, madawa
ya kulevya, riba, zinaa, fitina, kutukana, dharau, kukata udugu, ushirikina, kutosali,
kutowatii wazazi /walezi na walimu, wizi, ujambazi, muziki, kuvaa nusu uchi na mengine
yaliyoharamishwa, kushiriki katika mchakato wa kufanikisha utekelezaji wa mambo hayo.
Hivyo, kwa muktadha huo, elimu ni mchakato wa mabadiliko ya tabia, kutoka kwenye hali
duni kiutendaji na kuelekea kwenye ufanisi. Pia, msomi aliyeelimika ni yule aliyebadilika
tabia na mwenendo wake kutoka katika hali duni kiutendaji, kuelekea hali ya ufanisi,
kutokana na ujuzi alioupata darasani au nje ya darasa, vitabuni au katika mazingira
yaliyomzunguka. Ni katika maana hii Allah (S.W) anawafahamisha wanadamu kupitia
Qur’an kwa kusema:
َ
ْ ْ ُ ُ َّ َ َ َ َ َّ َ َ َ َّ َ َ َّ َ ْ َ ْ َ ْ ُ
ُ ْ َ
َ
ُ ْ َ َ
ُ
َ
َ
٩باللا ولوأ ركذتي امنِإ نوملعي ل نيِلاو نوملعي نيِلا يوتسي له لق
ِ
ِ
“...Sema: Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?
Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.” (Az-Zumar, 39:9)
Katika aya hiyo, Allah (S.W) anadhihirisha kuwa mjuzi na asiyejua hawawezi kuwa sawa
kiutendaji na kitabia. Utendaji wa mtu mwenye ujuzi sahihi ni wenye mafanikio, na pia
tabia yake huwa ni nyoofu, yenye kulingana na hadhi ya mwanadamu.
Malengo ya elimu
Ili kuona kwa upana zaidi malengo ya elimu, ni vema kutazama kwa ujumla mifumo ya
elimu ya Ujamaa na Ubepari, kisha kuilinganisha na mfumo wa kipekee wa Uislamu.
3