Page 12 - EDK_F5
P. 12
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
Kazi ya 1 1
Shirikiana na wanafunzi wenzako kuchunguza kielelezo namba 1 1 na kujadili
mafunzo yatokanayo
FOR ONLINE READING ONLY
Maana na malengo ya elimu
Sehemu hii, imeangazia tofauti za kimaana na kimalengo baina ya mfumo wa elimu wa
Uislamu na mfumo wa elimu wa Ujamaa na Ubepari. Imeangaziwa mifumo ya elimu ya
ujamaa na Ubepari, kwa sababu hii ndio mifumo mikubwa inayofuatwa na ulimwengu,
hasa kutokana na ushawishi wa mataifa makubwa yanayobeba kampeni ya mifumo hiyo.
Maana ya elimu
Wanazuoni wameeleza maana ya elimu katika mitazamo mbalimbali, inayoakisi matumizi
na mchakato wa upatikanaji wake. Baadhi yao wameeleza kuwa elimu ni ujuzi na
maarifa anayopata mwanafunzi kutoka kwa mwalimu. Wengine wameeleza kuwa elimu
ni utaratibu wa mafunzo, maelekezo, maarifa, uwezo, maendeleo ya tabia na nguvu za
kiakili zinazotokana na mafunzo hayo. Pia, wengine wameeleza kuwa elimu ni sanaa ya
kutengeneza mwanadamu. Vilevile, wengine wameeleza kuwa elimu ni mabadiliko ya
tabia, yanayotokana na maarifa aliyopata katika mchakato wa kujifunza. Kwa ujumla,
elimu ni mabadiliko ya tabia yanayotokana na ujuzi.
Wanazuoni wengi katika kueleza maana ya elimu, wameishia kuihusisha elimu na
kujenga akili ya mwanadamu katika ulimwengu wa kivitu na kusahau roho. Wakati roho
ndio msingi mkuu wa maadili katika jamii. Pia, mifumo ya elimu imezingatia hili kwa
kuhakikisha mwanadamu anawezeshwa kupata elimu itakayomsaidia kupata maendeleo
ya vitu bila kujali maadili yenye kunyanyua utu na heshima yake.
Uislamu unaitazama elimu kuwa ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Ujuzi ambao
unampatia msomaji msukumo wa kutenda kwa ufanisi, kwa kuzingatia maelekezo ya
Allah (S.W), kutokana na kuimarika kwa mahusiano baina ya nafsi ya mwanadamu na
dhati ya Allah (S.W). Maelekezo ya Allah (S.W) katika kutekeleza maisha ya kila siku,
yanapatikana kupitia Qur’an na Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W). Maelekezo hayo
yanamwezesha mwanadamu kuwa bora katika jamii na kukuza utu, heshima na maadili
yake.
Elimu haiishii katika kujua, kunakotokana na kujifunza au kufundishwa, bali elimu
hukamilika pale inapomwezesha mwenye kujua kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko yule
asiyejua. Aliyesoma bila kutafsiri alichokisoma katika matendo ya kila siku, ni sawa tu
na asiyesoma, kwa sababu wote hawa hawainufaishi jamii. Katika hali hii, msomi huyu
2