Page 11 - EDK_F5
P. 11
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
Sura ya kwanza
FOR ONLINE READING ONLY
Elimu katika Uislamu
Utangulizi
limu ni utambulisho wa dini ya Uislamu kwa kuwa ndio ufunuo wa kwanza
kumshukia Mtume Muhammad (S.A.W). Hivyo, Muislamu analazimika
Ekutafuta elimu kwa juhudi kubwa, kwani hawezi kutekeleza Uislamu kikamilifu
pasi na elimu. Katika sura hii utajifunza kutofautisha maana na malengo ya elimu baina
ya Uislamu na itikadi nyingine. Kisha, utajifunza kubainisha nafasi na umuhimu wa
elimu. Pia, utajifunza kubainisha dhana potofu kuhusu elimu na athari zake. Vilevile,
utajifunza kuchambua mchango wa Waislamu katika taaluma. Inategemewa kuwa baada
ya kumaliza sura hii utaweza kuishi kwa mujibu wa itikadi ya Uislamu.
Kielelezo namba 1.1: Safari ya elimu.
1