Page 162 - EDK_F5
P. 162
SURA YA TANO KUFASIRI QUR’AN
Nne, pia wanazuoni wa zama za Tabiin, walijiepusha sana kufafanua aya fiche
(Mutashabihat) katika Qur’an.
Tafsir ya Qur’an katika zama zilizofuata
Historia ya tafsir ya Qur’an katika zama zilizofuata (baada ya Tabiin), ilishuhudia juhudi
FOR ONLINE READING ONLY
mbalimbali zilizofanywa na kuendelezwa kimaandishi, kutoka katika misingi iliyowekwa
na watangulizi wao. Kipindi hiki kinagawanyika katika hatua nne zifuatazo:
Hatua ya kwanza, Muhaddithun (Wanazuoni wa Hadith) kama vile Shu’bah ibn Hajaj,
aliyefariki mwaka 160H/ 782 M, Waki’i ibn Jar’rah aliyefariki mwaka 197H/ 819M.
Katika juhudi zao, walikuwa wakijumuisha simulizi mbalimbali za tafsir za aya za Qur’an,
zilizonasibishwa na Mtume Muhammad (S.A.W) au Maswahaba zake au Tabiiin.
Hatua ya pili, katika juhudi zilizofanywa baadae (baada ya Tabiin), kuhusu tafsir ya
Qur’an, ilikuwa ni kupangwa kwa tafsir. Katika hatua hii tafsir mbalimbali za aya
zilipangwa na kuandikwa kwa kutenganishwa na Hadith, zikiwa pamoja na silsila ya
wasimulizi wake (Sanad). Miongoni mwa wanazuoni waliojitokeza katika kuifanya kazi
hiyo, ni pamoja na Ibn Jarir Twabari aliyefariki mwaka 310H na mwishoni mwa zama hizi
alijitokeza Abu-Bakr Ibn Mardawah, aliyefariki mwaka 410H.
Hatua ya tatu, katika tafsir ya Qur’an, ilitegemea vyanzo vyote walivyotumia
watangulizi wao (Tabii tabiin), pamoja na simulizi ambazo miongoni mwao zilikuwa
sahihi na zisizo sahihi (Hadith dhaifu), na wakaondoa silsila ya wapokezi. Kwa maana
katika uandishi, walikuwa wakieleza maoni ya watangulizi wao, bila kuwataja kuwa wao
ndio waliosema na waliyatoa wapi. Kwa sababu hiyo, zikaenea simulizi nyingi za watu
wa kitabu (Israiliyat) katika Tafsir walizoandika.
Hatua ya nne, Tafsir ilitegemea sana ushawishi wa mfasiri na taaluma aliyokuwanayo,
aina ya kipawa chake na madhehebu yake. Mambo hayo yalishawishi sana tafsir hadi
ikaenda mbali zaidi katika fani ndogondogo za lugha, ambazo mfasiri amebobea. Mwendo
huu wa tafsir ndio uliondelea hadi sasa.
Zoezi la 5 1
1. Onesha uhusiano baina ya tafsir, taawil na tarjama
2. Kwanini tunahitaji tafsir ya Qur’an?
3. Bainisha sababu nne zilizopelekea Tabi’in kujiepusha kufasiri aya Mutashabihat
4. Fafanua dhana ya tarjama na namna inavyotofautiana na tafsir
152