Page 164 - EDK_F5
P. 164
SURA YA TANO KUFASIRI QUR’AN
Sifa za tafsir Bil Maathur
Tafsir Bil Maathur ni bora kuliko ngazi zote za tafsir kwa kuwa:
a) inazingatia ufafanuzi kutoka katika vyanzo vya msingi visivyo na wasiwasi wa
upogo;
FOR ONLINE READING ONLY
b) inabainisha aya za Qur’an zilizo jumla (mujmal) kwa kutumia aya zingine zilizo
wazi au mahususi (mubayyan);
c) inabainisha aya zilizoachwa huru (mutlaq) kwa zingine zilizofungwa (muqayyad);
d) inabainisha aya za Qur’an zilizo na maelekezo ya jumla (‘amm) kwa zingine zilizo
na maelekezo mahususi (khas);
e) inaondoa changamoto inayoonesha kuwepo kwa kukinzana baina ya aya moja ya
Qur’an na nyingine;
f) inafafanua vema na kutofautisha baina ya aya zinazofuta (Nasikh) na aya zilizofutwa
(Mansukh);
g) inabainisha maelekezo mbalimbali ya kisharia yaliyopo katika baadhi ya aya
(Aayat Ahkam), ambazo hazina ufafanuzi. Kama vile aya zinazoeleza twahara,
Funga, Zakat na Hijja; na
h) inaangalia ufafanuzi uliotolewa katika Sunnah, athari za maswahaba na historia,
ambayo baadaye ilikuja kutambuliwa kama sababu ya kuteremshwa kwa aya
husika.
Udhaifu katika tafsir Bil Maathur
Pamoja na ubora usio na shaka wa ngazi hii ya Tafsir, lakini bado wanazuoni walibaini
udhaifu katika baadhi ya maeneo, hasa ikizingatiwa upana wa maudhui ya Qur’an,
yanayoenea kila nyanja ya maisha na katika mazingira yote. Miongoni mwa nukta
zinazoonyesha udhaifu katika ngazi hiyo ya Tafsir ni pamoja na:
(a) Mwanzoni, Tafsir Bil Maathur ilisomeshwa kama sehemu ya fani ya Hadith kabla
haijatenganishwa, hivyo ilizingatia pia vigezo vya isnad na matin kama Hadith.
Kwa sababu hiyo, haiwezi kukosa kasoro kabisa kwa kuwa katika Hadith pamoja
na kuwepo kwa vigezo hivyo bado zinabainika Hadith Sahihi, Hasan na Dhaifu
pia, bali hata Maudhuu. Kwa kuwa tafsir hii ilipita katika njia hizo bila shaka
simulizi zake hazitakosa madaraja hayo.
154