Page 168 - EDK_F5
P. 168
SURA YA TANO KUFASIRI QUR’AN
ya sababu au chanzo. Na neno Nuzul lina maana ya kuteremshwa au kushushwa. Hivyo
Sababun Nuzuul kwa ujumla wake ni somo linalohusu sababu za kuteremshwa kwa
aya mbalimbali za Qur’an; au ni ujuzi kuhusu matukio fulani ya kihistoria, ambayo
yanahusishwa na kushuka kwa ibara, sura au aya fulani za Qur’an.
Umuhimu wa Sababun nuzuul
FOR ONLINE READING ONLY
Haiwezekani kuwa na maarifa ya kufasiri aya za Qur’an vilivyo, bila kujishughulisha na
simulizi au maelezo yanayoeleza sababu ya kushuka kwake. Hivyo, kufahamu kuhusu
Sababun Nuzuul kunasaidia kuelewa vema mazingira ambayo aya husika ilishuka. Kwa
kujua mazingira ya kushuka, inatoa nafasi kwa mfasiri kujua kuwa aya hiyo, ilimaanisha
nini na kutoa mwongozo wa kuifafanua na kujua matumizi yake mengine, katika hali
tofauti.
Kwa ujumla, ujuzi wa Sababun nuzuul unamsaidia mtu kwanza kuelewa; maana ya
moja kwa moja na ya kiutendaji kwa kuwa itajibainisha kutoka katika mazingira halisi.
Pili, sababu inayojitokeza katika kushuka kwa aya huwa inakuwa na hukumu ya kisharia.
malengo halisi ya aya, kujua kama aya hiyo ni ya jumla au ni mahususi katika matumizi,
na katika mazingira gani inapaswa kutumika. Vilevile, kujua mazingira ya kihistoria
wakati wa Mtume Muhammad (S.A.W) na maendeleo ya jamii ya Kiislamu.
Kujulikana kwa Sababun nuzuul
Sabubun nuzuul zinazofahamika na kuaminiwa ni zile zilizosimuliwa na Maswahaba
wa Mtume Muhammad (S.A.W). Aidha, zimechukuliwa pia simulizi zilizothibitishwa
kwa usahihi, kwa kuzingatia njia za usahihishaji wa Hadith. Miongoni mwa vigezo
vilivyoangaliwa ni kuwa msimulizi wa sababu hiyo, awe ni katika watu waliokuwepo
katika eneo ambalo aya husika ilishuka. Ama, simulizi kutoka kwa Tabi’in pekee, ambayo
haina muunganiko na Swahaba inadhoofishwa. Hivyo, hayakubaliki maoni binafsi ya
mtu yoyote kusemea kuwa aya fulani ilishuka kwa sababu fulani bila sanad iliyonyooka
inayomkuta Mtume Muhammad (S.A.W).
Aina za Asbabun nuzuul
Asbabun nuzuul ni wingi wa sababun nuzuul. Kuna aina tatu za Asbaabun nuzuul katika
aya za Qur’an ambapo ya kwanza ni kubainisha au kujibu matukio au hali ya jumla
iliyojitokeza. Pili, kujibu swali liloulizwa au hoja iliyoibuliwa na mtu au watu, na tatu ni
sababu nyinginezo tunazozijua na tusizozijua.
Kwanza, katika sababu ya kubainisha au kujibu matukio au hali iliyojitokeza katika jamii
kuna mifano mingi ikiwemo:
Tukio la Abu Lahab; kama anavyosimulia Ibn Abbas (R.A) kuwa Mtume Muhammad
(S.A.W) alitoka akielekea Al-Batha kisha akapanda mlima na kunadi “Enyi ndugu zangu;
mara Maquraysh wakakusanyika na kumuelekea. Kisha akasema: “Ikiwa nitawaambia
158