Page 169 - EDK_F5
P. 169
SURA YA TANO KUFASIRI QUR’AN
kuwa nyuma ya mlima huu kuna maadui wanakuja kuwashambulia asubuhi au jioni
mtaniamini..? Wakajibu Maquraysh: “Ndio” basi akasema kuwaambia kuwa “Hakika
mimi ni mjumbe wa Allah (S.W) nimekuja kuwaonya na adhabu zake kali”. Akasema
Abu Lahab: “hivi ni kwa sababu hii kweli ndio umetukusanya hapa..? Uangamie kabisa
FOR ONLINE READING ONLY
ewe Muhammad..! kwa sababu hii Allah (S.W) akateremsha “Imeangamia mikono ya
Abu Lahab...” Surat Lahab, 111:1. Hadith imenukunuliwa na Imam Bukhari, VI, Na. 496.
Surat Lahab ilishuka kwa sababu ya tukio hili, baada ya Abu Lahab kubeza ujumbe wa
Mtume Muhammad (S.A.W) wazi wazi na kumtamkia maneno ya kumlaani mbele ya
kadamnasi. Hivyo, Allah (S.W) akamtakasa Mtume wake (S.A.W) na kumrudishia laana
yake Abu Lahab.
Tukio la Sa’i;
Kabla ya kusilimu Answar walikuwa wanahirimia ibada ya Hija kwa kuwataja masanamu
yao ambayo waliyaweka katika eneo la Mushallali. Baada ya kusilimu wakaona vibaya
kwenda Sa’i kati ya Safa na Marwa kwa kuchelea utajo wa masanamu yaliyokuwepo
kabla ya kusilimu.
Kwa sababu ya wasiwasi huo Allah (S.W) akateremsha aya ifuatayo:
ْ
َ
ْ َ َ َ ُ َ َ َ َ َ ْ َ َ ْ َ ْ َّ َ ْ َ َ َّ ٓ َ َ َ ْ َ َ َ َّ َّ
َ
ِهيلع حانج لف رمتعٱ وأ تيلٱ جح نمف ۖ ِللٱ رئاعش نِم ةورملٱو افصلٱ نِإ
ِ ِ
ِ
ٌ َ ٌ َ َ َّ َّ َ ً ْ َ َ َّ َ َ َ َ َ َ َّ َّ َ َ
١٥٨ ميِلع رِكاش للٱ نإف اۭيخ عوطت نمو ۚ امهب فوطي نأ
ِ ِ
ِ
Hakika Safa na Marwa ni katika ishara za Allah (S.W)...
(Al-Baqara, 2:158).
Pili, katika sababu ya kubainisha au kujibu matukio au hali iliyojitokeza katika jamii kuna
mifano mingi ikiwemo:
Swali kwa Mtume Muhammad (S A W) kuhusu mali; kuna matukio mengi ambapo
Mtume Muhammad (S.A.W) aliulizwa na Maswahaba zake (R.A) kuhusu Akida, na
hukumu mbalimbali za Kiislamu. Miongoni mwa waliyowahi kumuuliza na ukashuka
wahyi kubainisha ni swali la Swahaba Jabir (R.A) kama anavyosimulia katika Hadith
iliyopokelewa na Imam Bukhar kuwa: Anasimulia Jabir (R.A) kuwa: Mtume Muhammad
(S.A.W) na Abu Bakr (R.A) walikuja kwa mguu kuja kuniona nilipokuwa nikiumwa
katika makazi ya Banu Salama. Mtume Muhammad (S.A.W) akanikuta nikiwa
nimezirai, akaomba maji na kutia udhu, na kutoka katika maji yale akanirushia matone.
Nikazinduka na kusema “Ewe Mtume wa Allah (S.A.W)..! Unaniamrisha kufanya nini
katika mali yangu..? Hapo hapo ikashuka aya katika Surat Nisaa, 4:11 kuwa “Allah (S.W)
anakuamrisheni kuhusu urithi kwa watoto...” (Bukhar, VI, Na.101). Aya hiyo ilishuka
159