Page 170 - EDK_F5
P. 170

SURA YA TANO                                                           KUFASIRI QUR’AN

        kuleta sheria ya mirathi ya Kiislamu kwa watoto wetu, na hiyo ndio ilikuwa sababu ya
        kushuka kwake.

        Swali alilouliza  Mtume Muhammad  (S A W)  mwenyewe; katika tukio jingine,

        Mtume  Muhammad  (S.A.W)  aliuliza  swali  na  hatimaye  iliteremshwa  aya  ya  64  ya
        FOR ONLINE READING ONLY
        Surat Maryam,kujibu swali hilo, kama anavyosimulia Ibn Abbas (R.A) kuwa: Mtume
        Muhammad (S.A.W) alisema, “alimuuliza Jibril (A.S), kitu gani kinakuzuia wewe kuja
        kututembelea mara kwa mara? Kwa sababu hiyo ikashuka aya: Na hakika sisi (Malaika)
        hatushuki isipokuwa kwa amri ya Mola wetu. Hakika Yeye ndiye anaemiliki yaliyopo
        mbele yetu na nyuma yetu...” Surat Maryam, 19:64 (Bukhar, VI, Na.255)


        Hoja au swali la jumla katika jamii; katika  matukio  kadhaa  wahyi ulishuka  kutoa
        mwongozo  kuhusu maswali  au  hoja  za  jumla za  kijamii zilizoibuka katika umma  wa
        Kiislamu, anasimulia Thabit kutoka kwa Anas (R.A), ilikuwa katika jamii ya Wayahudi
        mwanamke akiwa katika hedhi, hawachanganyiki nae, wala hawaishi nae nyumba moja;
        Maswahaba (R.A) wakamuuliza Mtume Muhammad (S.A.W) kuhusu hilo, Allah (S.W)
        akateremsha aya ifuatayo: “Na wanakuuliza kuhusu hedhi; sema hiyo ni adha, kwa hiyo
        jiepusheni nao wakiwa katika hali hiyo...” (Surat Baqara, 2:222). Mtume Muhammad
        (S.A.W) akasema;  fanyeni  nao  mambo  yote  isipokuwa  jimai.  (Muslim,  I, Na.  592).
        Simulizi hii pia ni mfano mzuri wa Tafsir ya Mtume Muhammad (S.A.W) katika Qur’an

        baada ya kuulizwa.

        Swali au hoja ya mtu mmoja; sheria nyingi za jumla  ambazo  zimeelezwa  katika
        Qur’an zililetwa kama majibu ya mambo yaliyojitokeza katika jamii au majibu ya swali
        lililoulizwa na mtu binafsi. Mfano kushuka kwa aya katika Surat Baqara, 2:196

                                                                      ۡ
                ْ  ُ ۡ  َ  َ  َ  ۡ َ  ۡ  َ  َ َ ۡ َ ۡ  َ  َ  ۡ ُ ۡ  ۡ  ُ  ۡ َ  َّ َ َ ۡ ُ َ َّ َ  ۡ  ْ  ُّ َ َ
                اوقِلت لو ِۖ يدهلٱ نِم سيتسٱ امف مت ِ صحأ نإف ِۚ ِلل ةرمعلٱو جلٱ اومِتأو
                                                           ِ
                                                                   ُ
                  ّ   ٗ  َ  ٓ  ۡ  َ  ً  َّ  ُ  َ َ  َ  َ  ُ  َّ َ  ُ ۡ َ  ۡ  َ ۡ َ َّ َ ۡ ُ  َ ُ ُ
                                                                       ٰ
                نِم ىذأ ۦِهب وأ اضيرم مكنِم نك نمف  ۚ ۥهلِم يدهلٱ غلبي تح مكسوءر
                          ِ
                                  ِ
                 َ  َ ۡ ُ  ۡ  َ َّ َ  َ  َ  َ  ۡ ُ  َ  ٓ َ َ  ُ ۡ  َ  َ  َ َ ۡ  َ  َ  ّ َ ۡ َ  ۡ  َّ
                                                  ُ
                                                                        ٞ
                لِإ ِةرمعلٱب عتمت نمف متنِمأ اذإف ٖۚ كسن وأ ٍةقدص وأ ٍماي ِ ص نِم ةيدِفف ۦِهِسأر
                         ِ
                                            ِ
                 َ  َ ۡ َ َ ّ َ  ۡ  َّ  َ  َ َ َ  ُ َ  َ ۡ  َ َّ  َ  َ  ۡ َ  ۡ  َ  َ َ ۡ َ ۡ  َ  َ  ّ َ ۡ
                                                    ۡ
                                       ٰ
                                                 ِ
                اذِإ ٍةعبسو  ِ جلٱ  ِ ف ٖمايأ ِةثلث ماي ِ صف دي مل نمف ۚ ِ يدهلٱ نِم سيتسٱ امف  ِ جلٱ
                                           َ
                   ۡ      ۡ َ  ۡ     َ  ُ ۡ ۡ ُ َ ۡ  َّ  َ َ َ ٞ َ َ ٞ َ َ َ  ۡ  ۡ ُ ۡ َ َ
                                         ُ
                                                                    َ
                  َ َ
                                                            ٰ
                ِ
                ۚمارلٱ ِدجسملٱ ي ِ ضاح ۥهلهأ نكي مل نمِل كِلذ  ۗ ةلِمك ةشع كلِت ۗمتعجر
                        ِ
                                 ِ
                                                                    ٓ ُ ۡ َ َ َّ
                                                   َ  ۡ  ُ  َ َ َّ  َّ  َ  ْ َ  ْ  ُ َّ  َ
                                             ١٩٦ باقِعلٱ ديِدش للٱ نأ اوملعٱو للٱ اوقتٱو
                                                ِ
                Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na mkizuiwa,
                basi chinjeni wanyama walio wepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa
                vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao. Na atakayekuwa
                                                 160
   165   166   167   168   169   170   171   172   173   174   175