Page 165 - EDK_F5
P. 165
SURA YA TANO KUFASIRI QUR’AN
(b) Katika Tafsir Bil Maathur, ufafanuzi wa baadhi ya aya wafasiri wanatofautiana
katika kubainisha sababu za kushuka kwa aya.
(c) Ngazi hii ya Tafsir hapo mwanzoni ilibainika kuwa na simulizi za kiyahudi
na kikristo zilizochanganywa ndani yake. Hata hivyo, baadaye wanazuoni
FOR ONLINE READING ONLY
walibainisha na kuzitambulisha kwa jina la Israiliyat. Ibn Khaldun mmoja
kati ya wanazuoni hao, anasema katika kitabu chake Mukaddima kuwa; wengi
katika Wayahudi wa Yemen walioingia katika Uislamu walitoka katika kabila
la Himyar. Walipoingia katika Uislamu, bado walibaki na taarifa walizozipata
katika Uyahudi, kama vile habari za mwanzo wa uumbaji, matukio yaliyotabiriwa
kutokea hapo baadaye. Taarifa hizo hazikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na
Uislamu. Miongoni mwao walikuwemo Ka’ab ibn Ahbar na Wahb ibn Munabbih
na wengineo. Ufafanuzi waliotoa katika kusherehesha Qur’an ulikuwa na athari
ya simulizi hizo.
Tafsir Bil Ray
Ngazi ya pili ya Tafsir ya Qur’an ni tafsir Bil Ray. Hii ni aina ya tafsir ya maneno au
ibara au aya za Qur’an, kwa juhudi (ijtihad) ya kiakili (tafakuri), kwa kuangazia maana
ya kiasili ya aya, lugha iliyotumika, na muktadha.
Misingi ya tafsir Bil Ray
Tafsir Bil Ray ni zao la juhudi (ijtihad), inayofanywa kupitia katika vyanzo vinavyokubalika
kisheria. Misingi ya tafsir hii ni pamoja na:
a) Qur’an yenyewe na tafsir inayopatikana katika dhahiri yake;
b) Hadith za Mtume Muhammad (S.A.W) kuhusu jambo lililoelekezwa katika aya;
c) Athari za Maswahaba zinazonasibiana na aya au ibara ya Qur’an inayokusudiwa
kufafanuliwa;
d) Athari za Tabiin katika mwenendo wao wa maisha kulingana na aya husika;
e) Mazingira ya wakati uliopita, kipindi ambacho aya au sura husika imeteremshwa;
na
f) Mazingira yaliyopo hivi sasa.
155