Page 167 - EDK_F5
P. 167
SURA YA TANO KUFASIRI QUR’AN
iliyoandikwa mwanzoni na Imam Jalaluddin Al-Mahalli, aliyefariki mwaka 864 H na
baadaye kumaliziwa na Imam Jalaluddin Suyutwi, aliyezaliwa mwaka 849 H. Zingine
zilizoandikwa katika zama za karibuni na pamoja na Tafhim Al-Qur’an ya Sayyid Abu
A’la Mawdud na Fi-Dhilal Al-Qur’an ya Sayyid Qutb.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 5.4: Tafsir ya Imam Fakhruddin Al-Razi (Al-Tafsir al-Kabir)
Zoezi la 5 2
1. Bainisha tofauti nne kati ya Tafsir Bil Maathur na Tafsir Bil Ray
2. Toa hoja tano kuthibitisha stahiki ya Tafsir Bil Maathur kuwa katika ngazi ya
kwanza
3. Bainisha mambo matano yakipekee kuhusu Tafsir Bil Ray
Sababun nuzuul
Kazi ya 5 3
Katika vikundi someni matini ifuatayo kisha mueleze maana ya Sababun nuzuul na
umuhimu wake katika kuifasiri Qur’an
Qur’an imeteremshwa kuongoza watu katika muda na hali zote. Hata hivyo, baadhi ya
aya zake ziliteremshwa baada ya matukio fulani yaliyojitokeza katika wakati au zama
zilizopita. Neno sabab, ambalo wingi wake ni Asbaab ni neno la Kiarabu, lenye maana
157