Page 42 - EDK_F5
P. 42
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
hii ni jambo la kihistoria lenye kudumu ambalo pia limempatia mwandishi, heshima
na umaarufu duniani. Humo kuna kumbukumbu ya mambo ya kihistoria, juu ya aina
mbalimbali za ustaarabu duniani uliotokana na athari za mazingira na hali ya hewa tofauti,
maisha ya makazi ya kibedui (ya kuhamahama) na ya kudumu pamoja na tamaduni tofauti
tofauti za jamii hizo na pia taasisi tofauti za kijamii, sayansi na sanaa zao. Mwandishi pia
FOR ONLINE READING ONLY
anaongelea masuala ya sayansi, hesabu, muziki na ala zake, kilimo na sanaa kwa mujibu
wa Qur’an. Kwa kweli, ni kazi yenye maelezo kuhusu mambo mengi na yaliyoelezwa
kifasaha ambapo historia yenyewe imeelezewa kuwa ni sehemu ya somo la Falsafa kwa
maneno yafuatayo: “Hebu tutazame undani wa somo la Historia”, anasema Ibn Khaldun
kwamba, ni uchunguzi na uthibitisho wa taarifa, uchunguzi makini wa sababu za kuwepo
kwa mambo (kama yalivyo) na uelevu wa kina wa jinsi mambo yalivyoweza kutokea.
Hivyo, Historia ni mojawapo ya sehemu za somo la Falsafa, na inapaswa kutambuliwa
kama mojawapo ya elimu ya sayansi.” Hii kwa kweli ndiyo dhana ya kileo juu ya somo
la Historia, kutokana na kuuona umuhimu na nafasi yake katika uchambuzi wa taarifa
mbalimbali na kutafuta chanzo au sababu za mambo. Historia inapaswa kuwa ni elimu ya
kudumu katika ustaarabu wa mwanadamu na saikolojia yake.
Ni vigumu kuweza kuchambua kwa kina kazi kubwa aliyoifanya Ibn Khaldun.Uchunguzi
wake adilifu juu ya upoteaji na uharibifu wa staarabu mbalimbali, katika mzunguko, na
mchango mkuu wa wasomi katika uundaji wa mataifa mbalimbali, ambao amewanukuu
katika jitihada za kuhami dhana yake, ni mambo yenye kuvutia. Ibn Khaldun alibobea pale
alipoainisha maisha ya taifa lolote na ya watu au ya kiumbe kingine chochote, kwamba
hata mataifa yanazaliwa, yanakua na yanakufa. Pia, kwamba mataifa yako chini ya kanuni
ya mabadiliko asilia. Ibn Khaldun amehusika na uvumbuzi wa kanuni hii ya mabadiliko
ya taifa lolote.
Uchumi
Ibn Khaldun, mawazo yake ya kiuchumi kama ya kisiasa, yameendelea kutumika hata
leo. Mwandishi huyu kutoka iliyokuwa ikiitwa Maghreb (Morocco) anasema: “Taifa ni
sawa na mfanyabiashara mkubwa, kwani ana jukumu la kuhakikisha kuwa pesa azipatazo
kutokana na kodi, zinarudi na kuwazungukia watu. Kodi za wastani ni motisha tosha ili
watu waweze kujituma katika kufanya kazi. Kwa upande mwingine, kupandisha kodi
yoyote tena kiholela holela, kunaweza kusababisha yasipatikane mafanikio ya malengo
ya kodi husika.” Anachunguza kwa makini sana masuala ya utaifishaji au ushikiliaji wa
mali za watu, ukiritimba, usimamizi na udhibiti wa biashara kabla ya kuhitimisha kwa
kusema kwamba rasilimali za taifa, misingi yake mikuu ni watu, ari ya makampuni yake
32