Page 43 - EDK_F5
P. 43
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
ya kibiashara na tija katika ufanyaji wa shughuli zote za kiuchumi.
Kujiingiza kwa serikali katika utendaji wa shughuli za kiuchumi hupunguza uwezo
wa uzalishaji na utumiaji wa rasilimali za Taifa na hivyo huchelewesha upatikanaji wa
maendeleo katika jamii. Ukweli ni kwamba, taaluma ya siku hizi katika dhana ya uchumi
FOR ONLINE READING ONLY
huria haikuongeza lolote katika mtizamo kama huu, ambao ulishajengeka tangu karne ya
15.
Sehemu kubwa ya elimu hizi ilikuwa imehifadhiwa katika maktaba mbalimbali za umma
na binafsi. Palikuwa na vitabu vingi mno ukilinganisha na zama zenyewe; kwa mfano
Darul Hikma huko Cairo (karne 11) ilikuwa na vitabu milioni 1.6, Baitul Hikma, Baghdad
(karne ya 8) palikuwa na vitabu vingi sana, wakati maktaba ya Al-Hakm, Hispania ilikuwa
na vitabu laki 4 na ile ya Bani Ammar Tripoli ilikuwa na vitabu milioni moja.
Waislamu walipoanza kusahau jukumu lao la ukhalifa, na wakashughulishwa zaidi na
mambo ya anasa na wengine kuanza kuyaendea maisha ya kitawa, maadui walianza
kuichukua nafasi hiyo kidogo kidogo. Mgawanyo wa elimu nao ulipochukua nafasi yake,
Waislamu walianza kuwa duni na mara kuvamiwa na maadui zao. Wamongolia, kwa
mfano, walivamia Baghdad na kuvitupa vitabu vingi sana katika mto Trigis, hadi mto huo
kufurika na maji kugeuka rangi nyeusi, kwa sababu ya wino. Huko Hispania, ilipotekwa
Dola ya Kiislamu na Wakristo, vitabu milioni moja vilikuwa vikichomwa moto kila siku!
Vitabu vingine vilivyoandikwa na Waislamu vilitafsiriwa kwa lugha nyingine; Kifaransa,
Kilatini, Kiitaliana n.k hivyo Wazungu wakatumia nafasi hiyo kujidai uandishi.
Kilimo na viwanda
Katika fani ya kilimo na viwanda, aidha wanazuoni Waislamu walikuwa ndio viongozi. Ibn
Awwami aliweza kuainisha aina 585 za mimea, na kuitolea maelezo ya namna ya kuikuza.
Abu-Abbas An-Nabati (Abu Abbas, the Botanist yaani Abu Abbas, bingwa wa elimu ya
mimea), alikuwa akizunguka bahari ya Sham hadi Afrika, kukusanya aina mbalimbali
za mimea. Kwenye nchi ya Syria, kulikuwa na viwanda vya ufumaji, kutengeneza kauri,
nguo za pamba, ngozi, madini, glasi na vyuma. Elimu ya Kemia, ilitumika kutengeneza
marashi na mafuta mazuri kutoka kwenye maua ya waridi. Utengenezaji wa karatasi
ulikuwa umeshitadi kila upande, kwa kuwa huwezi kuhimiza kusoma bila ya kuwa na
zana za kuandikia.
33