Page 46 - EDK_F5
P. 46
SURA YA PILI ITIKADI KATIKA UISLAMU
Sura ya pili
FOR ONLINE READING ONLY
Itikadi katika Uislamu
Utangulizi
wa kawaida, kila mtu huwa na tabia ya kushikilia kitu fulani moyoni au akilini
mwake. Kitu hicho mbele ya macho ya wengine, kinaweza kuwa na thamani au
Kkisiwe na thamani, hilo si muhimu kwa mtazamo wa mhusika. Kwa kuwa mtu
ameshaamua kushikilia mawazo, fikra au maono fulani, huwa hana budi ila kuyaamini
na kuyafuata, maishani mwake. Aghalabu, mtu huyo akiamini na kufuata fikra fulani,
huwa ni vigumu kubadilika, hivyo, jambo hilo linaitwa itikadi.
Kwa maana hiyo, itikadi ni msimamo wa mtu juu ya maarifa ya kitu fulani, kwa
kukiamini na kukikubali kwa mtazamo wake, sawa kiwe na usahihi au makosa. Katika
Sura hii, utajifunza kuhusu tofauti kati ya itikadi ya Uislamu na itikadi nyingine na
athari zake. Baada ya kujifunza sura hii, unatarajiwa kupata umahiri wa kuthibitisha
usahihi wa itikadi ya Uislamu.
Tofauti za kiitikadi
Kazi ya 2 1
Shirikiana na wanafunzi wenzako kusoma aya hii, kisha jibu maswali yanayofuata:
َّ ۡ ُ َ ُ َّ ۡ ُ ۡ َ َ َ َ ّ ۡ َ ُ ۡ ُّ َ َّ َ َّ َ ّ َ َ ۡ ٓ َ
ۢ
ٰ
ِللٱب نِمؤيو ِ توغطلٱب رفكي نمف غلٱ نِم دشرلٱ ينبت دق نيِلدٱ ِ ف هاركِإ ل
ِ
ۖ
ِ
ۚ ِ
ِ
َ
ٌ َ ٌ َ ُ َّ َ َ َ َ َ َ ۡ ۡ ُ َ ۡ ُ ۡ َ َ ۡ َ ۡ َ َ
ٰ
٢٥٦ ميِلع عيِمس للٱو ۗاهل ماصِفنٱ ل قثولٱ ِةورعلٱب كسمتسٱ ِدقف
ِ
Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini. Uongofu umekwisha
pambanuka na upotofu. Basi anayemkataa shetani na akamwamini
Mwenyezi Mungu, bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu
kisichokuwa na kuvunjika. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia
mwenye kujua”. (Al-Baqara, 2: 256)
36