Page 49 - EDK_F5
P. 49
SURA YA PILI ITIKADI KATIKA UISLAMU
wa mifumo inayoundwa na mwanadamu. Hivyo, katika sehemu hii, zimeangaziwa tofauti
za itikadi katika sehemu kuu mbili:
a) Itikadi na madhara ya dini zilizobuniwa na wanadamu
b) Ubora wa Itikadi na usahihi wa dini ya Uislamu
FOR ONLINE READING ONLY
Itikadi ya Ukafiri
Ukafiri ni dini iliyojengwa kwa misingi ya kukana kuwepo kwa Allah (S.W), Muumba wa
viumbe vyote. Ukafiri unaitakidi mambo yafuatayo:
i. Hakuna Mungu Muumba wa vitu vyote ulimwenguni. Lakini viumbe vyote
vimetokea kwa bahati nasibu;
ii. Hakuna malengo na makusudio maalumu ya kuumbwa viumbe, hivyo mwanadamu
hana lengo ila kuishi tu. Kwa maana lengo la kuishi mwanadamu hapa duniani ni
kupata mahitaji ya maisha na kuendeleza maisha;
iii. Kwa kuwa hakuna Mungu Muumba wa ulimwengu, mwanadamu kwa ujuzi wake
alionao, ana jukumu la kujiundia mfumo wa maisha wenye manufaa kwake, ili
kuishi kwa amani na furaha hapa duniani; na
iv. Kwa kuwa mwanadamu na maumbile yote vimetokea kwa bahati nasibu, hivyo
mwisho wa maumbile yote ni kutoweka kwa bahati nasibu. Kwa maana nyingine
makafiri wanaitakidi kuwa hapana maisha mengine baada ya maisha ya hapa
duniani.
Itikadi hii imebainishwa bayana katika Qur’an, pale Allah (S.W) anaposema:
َ
ۡ
ۡ
َ
َ
ُ َ َ َ ُ َّ َّ ٓ ُ ۡ ُ َ َ َ ۡ َ ُ ُ َ َ ُّ َ ُ َ َّ َ َ ْ ُ َ َ
مهل امو ۚرهلدٱ لِإ انكِلهي امو اينو تومن اينلدٱ انتايح لِإ ِ ه ام اولاقو
َ ُّ ُ َ َّ ۡ ُ ۡ ۡ ۡ َ َ
ٰ
٢٤نونظي لِإ مه نِإ ملِع نِم كِلذب
ٍۖ
ِ
Na walisema: “Haukuwa (uhai) ila ni uhai wetu huu wa dunia,(hakuna
mwingine); tunakufa na tunaishi, wala hakuna kinachotuangamiza
isipokuwa (huu huu) ulimwengu; (kwani ndiyo ada yake kufisha na
kuhuisha).” Lakini wao hawana ilimu ya hayo (wanayoyasema)
wanadhani tu.” (Al-Jathiyah, 45: 24)
Madhara ya itikadi ya Ukafiri
Itikadi ya Ukafiri ina madhara katika jamii, yanayoweza kujumuishwa katika vipengele
vifuatavyo:
39