Page 47 - EDK_F5
P. 47
SURA YA PILI ITIKADI KATIKA UISLAMU
Maswali:
1. Aya hii inazungumzia kitu gani?
2. Unapata mafunzo gani kutokana na aya hii?
FOR ONLINE READING ONLY
Maana ya itikadi
Wataalamu wametoa maana mbalimbali za itikadi kwa mujibu wa mitazamo yao. Katika
uwanja wa sosiolojia, itikadi inarejelewa kama jumla ya maadili, imani, mawazo na
matarajio ya mtu. Itikadi ipo ndani ya jamii, makundi, na baina ya watu. Hubuniwa
mawazo, matendo, na utangamano wa watu, pamoja na kile kinachotokea katika jamii
kwa ujumla.
Ama kwa upande wa wanazuoni wa Kiislamu, itikadi wanaifasiri kuwa ni msimamo wa
mtu juu ya maarifa ya kitu fulani, unaofungamana moyoni kupitia imani, sawa uwe sahihi
au wenye makosa. Kwa mujibu wa wanazuoni wa Kiislamu, itikadi imejikita zaidi katika
masuala yanayofungamana na dini. Kwa muktadha huo, itikadi inajikita juu ya fikra na
imani za kidini sawa dini hiyo iwe sahihi au isiwe sahihi.
Aina za itikadi
Kazi ya 2 2
Shirikiana na wanafunzi wenzako kuchunguza kielelezo namba 2.1 na kutoa tafsiri ya
alama zilizomo katika kielelezo hicho
Kuna aina kuu mbili za itikadi: itikadi za wanadamu na itikadi ya Mola Mlezi. Katika
kundi la itikadi za wanadamu zilizo maarufu zaidi ni itikadi za kisiasa, na itikadi za
kiepistemolojia. Epistemolojia ni sehemu ya falsafa inayohusu utafiti wa jinsi mambo
yanavyojulikana.
Itikadi ya kisiasa, hujikita katika upangiliaji wa mawazo ya kimaadili na vipi nchi
iendeshwe.Wakati, itikadi za kiepistemolojia hujihusisha na upangiliaji wa mawazo ya
kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu wanapaswa kufanya maamuzi. Kwa muktadha
huo, katika itikadi za wanadamu, kunapatikana aina nyingine ndogondogo za itikadi.
Moja kati ya hizo ni pamoja na Ukomunisti, Usoshalisti na Ubepari; itikadi hizo hujikita
katika nyanja za kiuchumi na kisiasa kwa ujumla. Kwa kuwa itikadi zote zinahusisha
mwanadamu na maisha yake, mwanadamu huchagua aina moja au zaidi katika kuendesha
37