Page 48 - EDK_F5
P. 48
SURA YA PILI ITIKADI KATIKA UISLAMU
maisha yake. Hivyo, itikadi inafungamana na mfumo wa maisha, ambao ndio dini. Dini
zenyewe zimegawika katika makundi makubwa mawili:
(i) Dini ya Allah (S.W) inayojulikana kwa jina la Uislamu, na
(ii) Dini zilizoundwa na wanadamu, ambazo nazo zimegawika katika makundi makuu
matatu yafuatayo:
FOR ONLINE READING ONLY
a) Dini ya Ukafiri
b) Dini ya Ushirikina
c) Dini ya Utawa
Kielelezo namba 2.1: Nembo za Itikadi.
Tofauti za itikadi na athari zake
Itikadi za dini zilizobuniwa na wanadamu zina madhara mbalimbali, kwa kuwa zimebuniwa
na kiumbe mwenye udhaifu, katika milango anayoitumia kutafakari na kutolea maamuzi;
macho, masikio, ngozi, ulimi, na akili. Ukiachana na udhaifu huo, pia mwanadamu
ametawaliwa na matamanio ya nafsi, hivyo chochote anachokibuni huwa kwa lengo la
maslahi yake binafsi. Hana tabia ya kuwanufaisha wengine. Hii nayo ni sababu ya udhaifu
38