Page 45 - EDK_F5
P. 45
SURA YA KWANZA ELIMU KATIKA UISLAMU
Zoezi la marudio la 1
1. Fafanua faida za kusoma kwa kuzingatia malengo ya elimu katika Uislamu
2. Mifumo ya elimu inayotokana na mifumo ya maisha iliyobuniwa na wanadamu
FOR ONLINE READING ONLY
ina changamoto. Fafanua kauli hiyo kwa kurejea mfumo wa elimu wa Ujamaa na
Ubepari
3. Kwa mujibu wa Uislamu, eleza madhara matano ya kuitumia elimu nje ya lengo
lake
4. Chambua sifa tatu zinazobainisha elimu yenye manufaa katika jamii
5. Fafanua madhara matano ya mgawanyo wa elimu ya dini na elimu ya dunia katika
jamii inayokuzunguka
6. Baadhi ya watu katika jamii wanadai kwamba chimbuko la fani za elimu zilizopo
duniani zimetokana na mwanadamu mwenyewe. Thibitisha au kanusha madai hayo
kwa kutumia hoja tano
7. Bainisha mchango wa Waislamu katika maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa
kuzingatia fani zifuatazo:
(a) Unajimu
(b) Jiografia
(c) Hisabati
(d) Kemia
(e) Elimu ya Tiba
35