Page 176 - Fasihi_Kisw_F5
P. 176
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Uhariri: Kazi ya kusoma, kusahihisha na kusanifu miswada kama vile
makala au vitabu
Uigizaji: Tendo la kuchukua vitu kutoka nje na kuviingiza ndani ya
sehemu au eneo lenu jukwaa
FOR ONLINE READING ONLY
Ujumi: tathmini inayobainisha ubora au ubaya wa kazi za kisanaa
Ujuzi: Ufundi au utaalamu au maarifa alionayo mtu katika kufanya
shughuli fulani
Uketo/ utao: Kipande cha pili katika mshororo
Ukwapi: Kipande cha kwanza katika mshororo
Umahiri: Ni ujuzi mkubwa wa kufanya jambo fulani
Upeo: Ni mstari wa mwisho katika ubeti wa shairi
Usawiri: kutoa sura halisi ya kitu
Ushairi: Utanzu wa fasihi ambao hutumia sauti zilizopangiliwa, mizani,
lugha ya mkato, lugha ya mafumbo na uimbaji au ughani ili
kuwasilisha kwa hadhira maudhui yaliyokusudiwa
Utafiti: Uchunguzi wa kitaalamu wa jambo kwa kukusanya data na
kuzichambua ili kupata ukweli wa jambo fulani
Utamaduni: Mfumo wa maisha wa jamii fulani unaojumuisha mila, jadi,
desturi na sanaa za kundi la jamii fulani
Utanzu: Kundi linalojumuisha kazi mbalimbali za sanaa zenye kuchangia
sifa fulani kuu
Utendi: Utungo mrefu wa kishairi unaozungumzia kwa mapana matendo
ya kihistoria ya shujaa
Utenzi: Utungo mrefu wa kishairi unaohusu mawaidha au masuala
mengine ya kijamii
Utomeleaji: uchopekaji wa kipengele cha kipera fulani kwenye utanzu
tofauti. Mfano kipera cha nyimbo kikitumika kwenye riwaya au
hadithi fupi
Utunzi: Utungaji wa kazi yoyote ya kifasihi
Wimbo: Utungo wa kimuziki unaowasilishwa kwa kuimbwa na
huzingatia mahadhi maalum
Zana: Kitu ambacho mtu hukitumia kufanyia shughuli fulani
Kitabu cha Mwanafunzi 165
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 165 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 165