Page 174 - Fasihi_Kisw_F5
P. 174
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Nahau: Misemo ya picha ambayo huwa na maana iliyofichika. Kwa
kawaida, huundwa na kitenzi na nomino
Nathari: Utungo unaotumia lugha ya mjazo
Ngano: Hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama,
FOR ONLINE READING ONLY
miti na watu kuelezea na kuonya kuhusu maisha. Maudhui yake
hujikita katika maadili, mahusiano na mwenendo ndani ya jamii
Ngoma: Kipera cha sanaa za maonesho za jadi ambacho huhusisha
uchezeshaji wa viungo vya mwili wenye mtindo na miondoko
maalumu inayoambatana na muziki. Pia ni kifaa cha muziki
kilichowambwa kwa ngozi
Ngomezi: Fasihi itumiayo midundo ya ngoma ili kuwasilisha ujumbe
Ngonjera: Mazungumzo au majibizano ya kishairi ya kusemwa yanayohusu
mada fulani
Programu: Mfumo wa kompyuta ulioandaliwa kwa ajili ya kutenda kazi
fulani kama vile kutengeza vitabu, kupeleka au kupokea
baruapepe
Ramsa: Aina ya tamthiliya inayokusudia kufurahisha au kuchekesha, na
huwa na mwisho mwema
Riwaya: Hadithi ndefu ya kubuni itumiayo lugha ya kinathari (lugha ya
mjazo) na yenye uchangamani wa visa, wahusika, mandhari na
dhamira
Sanaa: Ufundi wa kuwasilisha hisia na mawazo ya binadamu kwa
maandishi, michoro, uchongaji, ufumaji na kadhalika
Sanifu: Weka taratibu za lugha zenye kufuata kanuni zinazokubalika
Shairi: Utungo wenye mishororo au mistari iliyogawanywa kwenye
mafungu kadhaa unaoeleza au kuonesha kwa ufupi wazo au
jambo au hisia fulani kuhusu binadamu na mazingira yake kwa
lugha ya picha na mkato
Sitiari: Tamathali ya usemi inayotumika kuonesha ulinganishi wa vitu
au hali tofauti bila ya kutumia maneno ya ulinganishi
Soga: Hadithi fupifupi za utani na ucheshi
Sokrate: Mwanafalsafa wa Kiyunani aliyeishi 469 - 399 K.K
Taashira: Tamathali ya usemi ambapo jina la sehemu ya kitu hutumika
kuwakilisha kitu kamili
Tabaini: Tamathali za semi inayosisitiza jambo kwa kutumia maneno au
kauli kinzani
Kitabu cha Mwanafunzi 163
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 163 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 163