Page 169 - Fasihi_Kisw_F5
P. 169
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(g) Taharuki
Hadithi za watoto hutumia taharuki ili kumtamanisha mtoto kufahamu tukio
linalofuata, kujua zaidi kuhusu matokeo ya mgogoro unaoendelea na kumfanya
adadisi zaidi kuhusu mtiririko wa hadithi hiyo. Mfano mzuri wa uundaji wa
FOR ONLINE READING ONLY
taharuki ni pale mhusika anapokuwa katika tukio la hatari ambalo mtoto hajui
hatima yake. Kwa hiyo, hutamani kusoma zaidi ili ajue mustakabali wake.
(h) Fantasia
Hadithi za watoto hutumia matukio, matendo na vitu visivyo vya kawaida, dhana
halisi na zile zenye maajabu ili kujenga taharuki na kuibua dhamira mbalimbali.
Mfano wa hadithi hizi ni pamoja na Marimba ya Majaliwa (Semzaba, 2008)
(i) Usimulizi
Usimulizi ni uwasilishaji wa kimfuatano wa matukio katika kazi ya fasihi kama
vile mashairi, tamthiliya, riwaya, hadithi fupi. Katika kazi nyingi za fasihi,
usimulizi wake ni wa nafsi ya kwanza au ya tatu. Vilevile, upo usimuliaji wa
nafsi ya pili. Katika tamthiliya, usimulzi hujitokeza katika mchanganyiko wa
maelekezo ya jukwaa na mazungumzo baina ya wahusika au hata mandhari au
muonekano wa wahusika.
(j) Dhamira zenye mafunzo chanya
Hadithi za watoto hupaswa kuwa na maudhui ya kuburudisha na yenye mafunzo
yanayowafaa. Kama ilivyo kawaida, dhamira huwa hazibainishwi wazi bali
msomaji hujenga maana kutokana na kile kinachosimuliwa. Hivyo, mtoto
anatakiwa kujengewa dhamira rahisi na kadri anavyokua ajengewe dhamira za
kufikirisha. Dhamira za watoto huweza kujengwa kwa kumfanya mtoto kutambua
vitu na mazingira, urafiki, mahusiano ya kifamilia, makuzi bora na kukabiliana
na hali tofauti za maisha.
Shughuli ya 6.12
Chagua mada moja kati ya zifuatazo, kisha tunga hadithi ya watoto kulingana
umri utakaochagua.
Mada za uandishi
(i) Safari ya ajabu
(ii) Maisha ya shule
(iii) Msitu wa ajabu
(iv) Watoto wa mtaani
(v) Mwanga wa elimu
158 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 158
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 158 23/06/2024 17:54