Page 168 - Fasihi_Kisw_F5
P. 168
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
na umri wao. Urahisi huo hutokana na sentensi kuwa fupi na uteuzi wa
msamiati unaoendana na kiwango chao. Vilevile, inashauriwa mwandishi wa
hadithi arudierudie maneno, sentensi na vifungu vya maneno ili kumsaidia
mtoto kuelewa suala linalowasilishwa. Hata hivyo, lugha inayotumika huweza
FOR ONLINE READING ONLY
kutofautiana kutokana na rika, umri na ngazi ya usomaji, kama vile ngazi ya
awali, shule za msingi na vijalunga chini ya miaka 18.
(b) Wahusika
Mara nyingi, wahusika ni watoto au wale wanaoakisi matendo ya rika lengwa,
yaani watendao au kuzungumza kitoto. Majina ya wahusika yasifanane wala
yasikaribiane ili kutokuwachanganya watoto. Kwa mfano si vizuri kwenye kazi
moja kutumia majina kama Avita na Avera, Paula na Paulo; Samiri, Samira na
Samri; au Petro, Petronia, na Petrobasi. Vilevile, ni vyema mhusika abainishwe
wazi kwa kuzingatia umbo, sifa, rangi, mavazi na tabia zake.
(c) Msuko wa visa na matukio
Hadithi za watoto hujengwa kwa msuko rahisi na wa moja kwa moja ambapo
kisa huwa na chanzo, kati na mwisho. Kwa mfano, mhusika anatambulishwa
akiwa anazaliwa, anasoma shule, mwisho anapata kazi. Vilevile, matukio yawe
na taharuki ili kuwavutia watoto kutamani kuendelea kusoma hadithi.
(d) Picha na michoro
Hadithi za watoto huwa na picha na michoro mingi kwa ajili ya kufafanua
zaidi maelezo, kuibua hisia, kurahisisha uelewa wa tukio linalowasilishwa,
kujenga kumbukumbu, kuongeza ubunifu na kuvutia watoto. Picha hizo huweza
kupambwa kwa rangi mbalimbali kutegemeana na maudhui na rika husika.
(e) Mandhari halisi
Mara nyingi, hadithi za watoto zinapaswa kusawiri miktadha ya kijamii
au kitamaduni inayowafaa watoto. Vilevile, mandhari za hadithi za watoto
zibainishwe wazi, zisiwe za kuwakatisha watoto tamaa ya kusoma suala
linaloweza kuwafanya washindwe kuendelea kuisoma hadithi. Inashauriwa
katika hadithi za watoto wadogo, rika la awali na kati, zitumike mandhari halisi.
(f) Taswira
Hadithi za watoto ziwe zinafikirisha na kuwajengea hisia na picha mbalimbali
akilini mwao ili kuwachangamsha. Taswira hujengwa kwa kutumia lugha ya
picha, tamathali za semi na mbinu nyingine za kisanaa zinazohusiana na umri
wao.
Kitabu cha Mwanafunzi 157
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 157 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 157