Page 172 - Fasihi_Kisw_F5
P. 172
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Kigano: Hadithi fupi ya fasihi simulizi ambayo hutolewa kwa kutumia
matumizi mapana ya ujadi
Kipera: Tawi la utanzu wa fasihi
Kisa: Masimulizi ya tukio la kweli lililotokea
FOR ONLINE READING ONLY
Kisasili: Hadithi inayoaminiwa kuwa kweli, inayoelezea chimbuko au
asili ya kitu na hufungamana na imani na miviga ya jamii
Kisasuli: Hadithi yenye kueleza usuli na sababu za jambo, tukio au hali
(yaani kwa nini jambo, tukio au hali iko kama ilivyo). Kisasuli
hakina uzito mkubwa kama kisasili, na si lazima kiaminiwe na
wanajamii.
Kitendawili: Usemi mfupi wa mafumbo wenye kutumia lugha ya picha,
tamathali na ishara katika kueleza jambo lililofichika
Lakabu: Jina au majina ya nyongeza au ya kupanga (ambayo sio halisi)
ambayo baadhi ya watu hupewa au hujipa kutokana na sifa zao
za kimaumbile, kinasaba, kitabia, kiujuzi au kimatendo
Lugha: Njia ya mawasiliano ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Mfano:
lugha ya maandishi, lugha ya masimulizi, lugha ya ishara, lugha
ya alama na lugha ya vitendo
Maghani: Tungo za kishairi zinazotongolewa kwa kutumia sauti iliyo kati
ya uimbaji na uzungumzaji
Maigizo: Sanaa inayotumia watendaji kuiga tabia na matendo ya watu au
viumbe wengine ili kuelimisha au kuburudisha
Majazi: Tamathali ya usemi ambayo wahusika wa kazi ya fasihi hupewa
majina yanayoakisi wasifu au tabia zao
Majigambo: Masimulizi ya kujisifia au kujikweza kwa mtu kuhusu mambo
anayoweza kuyafanya, aliyowahi kuyafanya au atakayoyafanya
Makala: Habari iliyoandikwa kueleza jambo mahususi kwenye gazeti,
jarida au kitabu
Maktaba: Mkusanyo wa machapisho kama vitabu, kanda, yaliyohifadhiwa
na ambayo huweza kuazimwa na kutumiwa
Maleba: Mavazi, vifaa na mapambo ya msanii anapokuwa jukwaani
Mandhari: Muonekano wa mahali unaojumuisha ardhi, miti, mito, milima
au mabonde
Maudhui: Jumla ya mambo mbalimbali yanayozungumziwa katika kazi
ya fasihi ambayo yanajengwa na dhamira, mtazamo, falsafa,
itikadi, msimamo, ujumbe, mafunzo na migogoro
Kitabu cha Mwanafunzi 161
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 161 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 161