Page 175 - Fasihi_Kisw_F5
P. 175
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Tafsiri: Ni uhawirishaji wa mawazo yaliyoandikwa kutoka lugha moja
hadi nyingine
Tahakiki: Andiko linalochambua na kufafanua kazi fulani ya fasihi
Taharuki: Hali ya kusisimua au wasiwasi kuhusu jambo fulani litakalotokea
FOR ONLINE READING ONLY
katika kipindi kijacho
Takhmisa: Shairi lenye mistari mitano
Takriri: Dhana inayotumika kuelezea hali ya kurudiarudia sauti, silabi,
neno au maneno
Tamthiliya: Mchezo ulioandaliwa kwa lengo la kuigizwa jukwaani
Tanakali lafudhi: Tamathali inayotumika kuonesha mwigo wa matamshi ya watu
fulani wanaotumia lugha kwa namna fulani
Tanakali sauti: Tamathali inayotumika kuonesha mwigo wa sauti za vitu
mbalimbali kulingana na lengo na muktadha husika
Taniaba: Tamathali ambayo hutumia jina la mtu binafsi kwa watu wengine
wenye tabia, mwenendo hali au kazi sawa na ya mtu huyo
Tarbia: Shairi la kimapokeo lenye mistari minne
Tarihi: Hadithi zinazohusu matukio muhimu ya kihistoria
Tasdisa/Sudusia: Shairi lenye mistari sita
Tashibiha: Tamathali inayotumika kuelezea hali ya ulinganishi kwa kutumia
maneno ya ulinganishi kama vile kama, mithili ya, mfano wa, na
sawa na
Tashihisi: Tamathali ambayo vitu visivyo na uhai na uwezo wa kutenda
hupewa uwezo huo
Tafsida: Lugha ya staha yenye lengo la kupunguza ukali au matusi katika
kauli
Taswira: Picha au jazanda inayojengwa akilini mwa hadhira anapoifuatilia
kazi ya sanaa
Tathlitha: Shairi lenye mistari mitatu
Tini: Muhtasari wa kumbukumbu za hoja au mawazo zinazoandikwa
kwa ajili ya kusomwa baadaye
Ubunifu: Uwezo wa kutafakari na kujenga fikra zinazounda na kufanya
kitu au jambo jipya lionekane
Uhakiki: Dhana inayohusika na kuchambua, kufafanua, kufasili,
kutathmini, na kueleza vipengele vya fani na maudhui katika
kazi za fasihi
164 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 164
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 164 23/06/2024 17:54