Page 171 - Fasihi_Kisw_F5
P. 171
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Faharasa
Akili mnemba: Mfumo wa kidijiti ambao umetengenezwa kwa ajili ya kutoa
majibu ya masuala mbalimbali
FOR ONLINE READING ONLY
Buni: Gugundua au tengeneza kitu kwa mara ya kwanza
Falsafa Elimu kuhusu asili, maana na sababu za mambo au vitu
Fani: Ufundi anaoutumia msanii katika kuwasilisha maudhui
Fantasia: Wazo la kufikirika lisiloweza kutekelezeka
Fumbo: Usemi au kauli ambayo maana yake haitolewi waziwazi bali
hufichwa
Fursa: Nafasi ya kuweza kufanya jambo
Futuhi: Aina ya tamthiliya inayokusudia kufurahisha au kuchekesha, na
huwa na mwisho mwema (Pia, ramsa)
Hadithi fupi: Simulizi ya kubuni inayosawiri tukio, tabia, mgogoro au
kipengele fulani cha maisha kwa ufupi, kwa kawaida, hadithi
fupi huwa na tukio moja au mawili na hutumia mawanda finyu
Hadithi za watoto: Tungo za kibunifu zinazowahusu watoto kifani na kimaudhui
Hadithi: Matukio yanayosimuliwa kwa mfuatano wa kimantiki na
kiwakati
Hekaya: Ngano zenye visa visivyo vya kawaida vinavyoambatana na
masaibu na pengine hata ujanja wa mhusika mkuu ambaye
huweza kuwa mtu au mnyama
Hurafa: Ngano zenye wahusika wanyama tu ambao huwakilisha tabia na
matendo ya binadamu kwa kurejelea masuala yanayopatikana
katika jamii ili kuwasilisha maana
Insha: Utungo mfupi wa kinathari (wa lugha ya mjazo) ambao
husimulia jambo kwa utimilifu
Istiara: Hadithi ambayo maana yake ya wazi inawakilisha maana
iliyofichika. Kwa hiyo, maana huwasilishwa kwa njia ya
mafumbo.
Itikadi: Jumla ya mfumo wa mawazo, fikra au imani inayoongoza na
kumwelekeza mtunzi katika kuwasilisha masuala mbalimbali
Jukwaa: Eneo maalumu lililotengenezwa kwa kuinuliwa juu ndani ya
jingo, ukumbi au uwanja ambalo hutumika kwa kutolea hutuba
au michezo
160 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 160
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 160 23/06/2024 17:54