Page 173 - Fasihi_Kisw_F5
P. 173
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mdokezo: Tamathali ambayo kitu fulani hudokezwa au huachwa bila
kukamilishwa, aghalabu, kitu hicho huwa kinafahamika katika
muktadha husika
Methali: Semi za kimapokeo zenye hekima na busara zinazotumia sitiari
kuelezea falsafa na uzoefu wa jamii fulani kwa muhtasari
FOR ONLINE READING ONLY
Mgogoro: Ni hali ya watu kukosa kukubaliana kuhusu suala fulani
inayoweza kusababisha mitafaruku
Mhadhiri: Mtaalamu au mwalimu wa taasisi ya elimu ya juu anayeelimisha
watu kwa njia ya mhadhara
Mhusika Bapa: Mhusika ambaye habadiliki kulingana na wakati, mazingira au
muktadha; yaani huonesha upande mmoja tu
Mila: Ni taratibu za kimaisha za mwenendo na jinsi ya kufanya mambo
zinzofuatwa na jamii fulani kulingana na historia na utamaduni
wao
Misingi: Chanzo au chimbuko la kitu fulani
Mitandao ya kijamii: Programu inayowezesha watu kuwasiliana kwa njia ya tovuti
au mfumo mwingine wa mawasiliano ya kielekitroniki
Miviga: Sherehe au shughuli za kijadi zinazofanywa na jamii katika
kipindi maalumu cha mwaka au katika muktadha maalumu
Mkondoni: Kuwa katika hali ya kuunganishwa na mtandao kupitia kompyuta
au vyombo vingine kidijiti
Mleo: mstari wa tatu wa shairi la beti za mistari mitatumitatu
Mloto: mstari wa pili katika ubeti wa shairi
Mtandao: Mfumo wa mawasiliano ya kielektroniki unaopitia katika
kompyuta ulimwenguni unaotumiwa kutafuta taarifa kuwasiliana
au kupeana taarifa
Mtazamo: Namna au jinsi mtu anavyochukulia kitu au jambo kisiasa au
kiuchumi
Mtindo: Kipengele cha kifani kinachohusu upekee au utofauti wa msanii
unaojitokeza katika kazi ya fasihi na hutokana na matumizi ya
lugha na vielelezo. Mtindo humtofautisha msanii mmoja na
mwingine katika kazi moja na nyingine
Muundo: Kipengele cha kifani kinachohusu umbo au mwonekano wa kazi
ya sanaa
Mwandamizi: Kipande au mgao wa tatu katika mshororo wa shairi ambalo
mishororo yake imegawanyika katika vipande vitatu
162 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 162
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 162 23/06/2024 17:54