Page 167 - Fasihi_Kisw_F5
P. 167
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(f) Utoshelevu
Ni muhimu shairi liwe na mtiririko mzuri wa mawazo unaolandana na mpangilio
wake. Mpangilio huo ndio unaoleta utoshelevu. Utoshelevu ni kanuni ambayo
inautaka kila mshororo na kila ubeti kujitosheleza kimaana ili kulifanya shairi
FOR ONLINE READING ONLY
likamilike kifani na kimaudhui.
Shughuli 6.10
(a) Soma mashairi mawili kutoka katika diwani teule kisha chambua kanuni
zilizotumika katika utunzi wake.
(b) Chagua mada unazozipenda kisha tunga mashairi mawili yasiyopungua beti
kumi (10) kwa kila shairi.
Shughuli ya 6.11
(a) Chunguza vitabu teule vya hadithi za watoto, kisha eleza maana na sifa za
hadithi hizo.
(b) Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni, maktabani au kwingineko, jadili
kanuni za utunzi wa hadithi za watoto.
Kanuni za kutunga hadithi za watoto
Hadithi za watoto ni aina ya kazi za fasihi zilizobuniwa kwa ajili ya watoto. Visa
na matukio, lugha, wahusika, michoro na picha, na maudhui yanayowasilishwa
katika hadithi za watoto huakisi hisia na akili za watoto. Hadithi hizi huwa na
sifa ambazo ni tofauti na hadithi za watu wazima ama hadithi nyingine. Hadithi
za watoto huweza kuwa na maandishi yenye ukubwa tofauti kulingana na umri
wa watoto, utofauti wa nafasi kati ya mstari na mstari, nakshi ya rangi, picha na
michoro, kurasa chache, lugha rahisi na wahusika wachache kulingana na umri
wa watoto.
Licha ya upekee wa hadithi za watoto lakini hatua za uandishi huwa ni sawa na
za kazi nyingine za kifasihi. Vilevile, vipengele vinavyojenga hadithi za watoto,
kama vile, lugha, wahusika, msuko wa visa na matukio huwa sawa na kazi
bunilizi nyinginezo kama vile hadithi fupi na riwaya. Pamoja na mfanano huo,
utunzi wa hadithi za watoto huongozwa na kanuni zifuatazo:
(a) Lugha
Hadithi za watoto hutumia lugha rahisi, inayoeleweka na ya kisanaa. Sanaa
katika lugha ya watoto hujumuisha semi, tamathali za semi na methali kulingana
156 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 156
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 156 23/06/2024 17:54