Page 164 - Fasihi_Kisw_F5
P. 164
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Zoezi la 6.3
1. Jadili kauli kuwa “uandishi wa kazi za kifasihi ni mchakato usiohitaji
utaratibu”.
FOR ONLINE READING ONLY
2. “Maandalizi ni hatua muhimu kabla ya uandishi wa kazi ya fasihi”.
Jadili.
3. Kwa kutumia mifano eleza masuala muhimu ambayo hufanyika katika
hatua ya kuboresha.
4. Tofautisha hatua ya uhariri na ya mapitio ya mwisho katika utunzi wa
kazi za kifasihi.
5. “Mapitio ya mwisho ni hatua inayompotezea muda mwandishi.” Jadili.
Shughuli ya 6.7
(a) Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni, maktabani na vinginevyo, eleza
maana na kanuni zinazoongoza utunzi wa maigizo.
(b) Angalia au sikiliza maigizo kutoka katika vyanzo mbalimbali, kisha
chambua kanuni zilizotumika katika utunzi wa igizo mojawapo.
Kanuni za kutunga maigizo, mashairi na hadithi za watoto
Utunzi wa kazi yoyote ya kifasihi huongozwa na kanuni maalumu ambazo
hutumika katika kutunga kazi za utanzu husika. Ufuatao ni ufafanuzi wa kanuni
za kutunga maigizo, mashairi na hadithi za watoto.
Kanuni za kutunga maigizo
Maigizo ni kipera cha sanaa za maonesho ambacho ni miongoni mwa tanzu za
fasihi simulizi. Maigizo ni sanaa ya kuwasilisha jambo au tukio kwa kutumia
lugha na vitendo. Mara nyingi maigizo hutendwa kwenye jukwaa la maonesho au
mahali popote maalumu mbele ya hadhira husika. Maigizo yanahitaji kutungwa
kwa ustadi ili kuwakonga watazamaji. Hatua za utunzi wa maigizo kwa kiasi
kikubwa zinafanana na zile za utunzi wa kazi nyingine za kifasihi isipokuwa
utunzi wa maigizo hujumuisha vipengele muhimu vinavyopatikana katika
maigizo tu. Kanuni muhimu za kuzingatiwa katika utunzi wa maigizo ni pamoja
na hizi zifuatazo:
Kitabu cha Mwanafunzi 153
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 153 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 153